


Benki
ya CBA yaja na huduma za kisasa za kibenki Katika mkakati wake wa
kuendelea kuboresha huduma zake nchini,Benki ya CBA imezindua huduma
mpya kwa wateja wake binafsi zitakazowawezesha kupata huduma za kibenki
kwa njia ya teknolojia ya kisasa ya kupata huduma za kibenki kimtandao
kupitia simu zao za mkononi. Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hii
mpya,Afisa Mtendaji Mkuu wa CBA Tanzania,Dk.Gift Shoko,alisema kuwa
huduma hizi zimelenga kuwarahisishia maisha wateja na kuwawezesha kupata
huduma za kibenki kulingana na matakwa yao na kwenda sambamba na mtindo
wa maisha wanaoishi.
Alisema
pia wateja wa CBA Tanzania kuanzia sasa wanaweza kutumia kadi za
kimataifa za kufanya mihamala ya malipo za Visa Platinum Debit Card na
Visa Gold Credit Card kwa fedha za kitanzania na Dola za Kimarekani
ambazo zinawawezesha kupata huduma mbalimbali wakiwa katika uwanja wa
ndege wa JKIA kwenye sehemu ya kupita watu maarufu (VIP lounge).Alisema
huduma hii itawawezesha wateja wa kundi hili kufanya mihamala wakiwa
katika viwanja vya ndege 600 kwenye nchi 1,000 na miji mikubwa ipatayo
300 duniani kote.
“Tunazidi
kurahisisha huduma za kibenki kwa wateja ili wazipate popote na kwa
wakati wowote watakapokuwa bila kupoteza muda kama ilivyokuwa hapo
awali”.Alisema. Kitengo cha kuhudumia wateja watakaojiunga na huduma hii
kwa kuanzia itapatikana jijini Dar es Salaam katika matawi yaliyopo
kwenye mitaa ya Ohio na Samora vilevile katika tawi la Arusha. Benki ya
CBA Tanzania ambayo ni moja ya Benki kubwa zinazoongoza kwa ubunifu wa
huduma mbalimbali za kibenki kwa wateja wake ,moja ya huduma ambayo
imeianzisha na kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya makazi ya kutoa
mikopo ya nyumba inayolipwa hadi kufikia kipindi cha miaka 20.
Benki
ya CBA Tanzania hadi kufikia sasa inayo matawi 11 nchini kote ambapo 5
yapo jijini Dar es Salaam na mengine katika miji ya Mbeya, Tunduma,
Mtwara, Moshi, Mwanza, na Arusha.Pia benki ipo katika nchi nyingine za
Afrika Mashariki za Kenya,Uganda na Rwanda ambazo ziko chini ya mwamvuli
wa CBA GROUP.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni