Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Hassan Kimanta
Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Monduli wakiwa kwenye kikwo cha pamoja.
Mahmoud Ahmad ...MONDULI.
Mkuu
wa wilaya ya Monduli Idd Hassan Kimanta ameliomba baraza la madiwani
kumpa usirikiano katika utendaji kazi ambapo ametoa siku 14 kwa
mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha anakusanya fedha za viwanja
vilivyopo Chuo Cha Maendeleo ya Jamii (CDTI) zaidi ya Shilingi milioni
700 ambazo zitatumika katka miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.
Agizo
hilo amelitoa wakati akizungumza kwenye baraza la madiwani monduli na
kumuagiza mkurugenzi kuwa fedha hizo zilipwe ndani ya siku 14 na
atakayeshindwa kulipa anyang'anywe mara moja na kurudishwa ofisini kwa
mkuu wa wilaya na amesema ifikapo jumatano orodha ya watu wenye viwanja
hivyo iwasilishwe ofisini kwake, ikiwa na idadi ya waliolipa na ambao
bado hawajalipa.
Aidha
amemtaka mkurugenzi kubandika matangazo maeneo mbalimbali ya wilaya
hiyo kuwataka wananchi wanaomiliki viwanja hivyo kuilipa halmashauri
hiyo fedha wanazodaiwa ndani ya siku 14 vinginevyo zikipita siku hizo
hatua ya kuwanyang'anya itafuata.
"Nakuagiza
mkurugenzi hakikisha unakusanya sh milioni 700 za viwanja vilivyopo
CDTI ambavyo vimeuzwa na waliouziwa hawajailipa halmashauri, hadi sasa ,
wengine wameshajenga na nyumba huku hawajalipa fedha hizo walipe ndani
ya siku 14 la sivyo wanyang'anywe alisisitiza Kimanta."
Sambamba
na hilo amewataka watumishi wote wa serikali kutimiza wajibu wao wa
kuwahudumia wananchi ipasavyo kuanzia ngazi ya kitongoji hadi wilaya na
ikitokea mwananchi anafika kwake wakati viongozi waliopo chini yake
hawana taarifa rungu litamshikia kiongozi husika .
Pamoja
na hayo amewataka watumishi wote kufika maeneo yao ya kazi saa moja na
nusu asubuhi siku za kazi na hakuna kuzurura ovyo hadi muda wa kutoka
ofisini saa tisa na nusu,huku akiwataka maafisa tarafa kufuatilia katika
maofisi mbalimbali ya utumishi wa uma kwani imeonekana kuna ofisi
nyingine watumishi wa uma hawafungui ofisi kuwahudumia ili wananchi
haswa vijiji hadi Kata wilayani humo.
WAKATI HUOHUO:
Mkuu
huyo amebainisha kuwepo kwa wanafunzi hewa katika shule za msingi na
sekondari katika wilayani Monduli ambapo wanafunzi hewa katika shule za
msingi ni 319 ,shule za sekondari 155 huku watoro katika shule ya msingi
wakiwa 353 sekondari 115 .
Kutokana
na hatua hiyo ya kubainika wanafunzi hewa katika shule za msingi na
sekondari serikali imeazimia kuwafukuza kazi walimu 8 wa sekondari na
waalimu 6 shule za msingi ambapo tatizo hilo limeisababishia serikali
hasara ya zaidi ya shilingi milioni 43.
Katika
kuhakikisha swala la elimu linaimarika amesema atahakikisha watoto
wakike wanasoma bila kubughudhiwa ,huku alipiga vita ndoa za
utotoni,pamoja na ukeketaji kwa watoto wa kike, kwani ni mila potofu
katika jamii nainasababisha madhara makubwa kwa watoto wa kike.
"Nawaomba
madiwani kwa vile nyie ni wanasiasa suala hili mniachie kwa vile nyie
ni msije kuharibu kura zenu,sijaja kupendwa Monduli wala sihitaji
zawadi ya mtu,mimi ndiyo natakiwa niwape ninyi wananchi zawadi ya
kuwatumikia ,na nipo tayari kufa kwajili ya kutetea haki yawannchi wa
Monduli alisisitiza Kimanta
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni