| Mkuu wa mkoa akipokea zawadi ya Cd kutoka kwenye chama cha wasanii wa filamu jiji la Arusha(TDFAA)kama shukrani kwa mcgango wake kwa chama hicho na wasanii wa Arusha kwa ujumla. | 
| Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Arusha Rebeka Mongi akiongea kwenye hafla hiyo. | 
| Mkuu wa mkoa na viongozi wa serikali mkoani hapa wakiwa wamesimama baada kupokea zawadi kutoka kwa wasanii wa filamu | 
| Kaimu mkurugenzi wa jiji la Arusha Rebeka Mongi akiongea neno kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kuzindua semina hiyo. | 
![]()  | 
| Mkuu wa mkoa akiongea na vyombo vya habari waliofika kwenye semina hiyo nje ya ukumbi baada ya kumaliza kufungua semina hiyo | 
| Mkuu wa mkoa Mrisho Gambo akiongozana na kaimu mkurugenzi wa jiji la Arusha Tebeka Mongi wakiwa wanaondoka | 
| Director wa filamu Fotnatus John akiimba mbele ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya semina ya Ujasiriamali na kuunda Saccoss kwa wasanii wa filamu jijini Arusha leo picha na mahmoud Ahmad Arusha 
SHIRIKISHO la wasanii wa filamu jijini Arusha washukiwa na Neema kutoka kwa Mkuu wa mkoa huo kutokana na mkuu huyo wa mkoa kuhaidi kutatua matatizo yao . 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameahidi kuwasaidia wasanii wa filamu Mkoani hapa ambapo amewataka kufika ofisini kwake mapema kesho  kwaajili  ya kuwasikikiza na kutatua kero zao. 
Akizungumza Jana  katika ufunguzi wa Mafunzo yaliyoandaliwa na jiji  hilo ya siku mbili yenye lengo la kuwafundisha vijana ujasiriamali na    jinsi ya kujikwamua katika umaskini Gambo aliwataka vijana kujiunga katika vikundi ili waweze kunufaika na asilimia tano  inayo toka serikalini. 
" Tunaamini  serikali yetu imekusudia kuwasidia wanyonge na wote wenye juhudi katika utafutaji hivyo ni vyema mkachangamkia fursa zitolewazo katika jamii yenu na mjiunge katika vikundi ambapo mtanufaika. alisema Gambo. 
Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la waigizaji wa filamu jijini Arusha(TDFAA) Isack Chalo  alisema  tasnia ya usanii mkoani hapo inakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo ukosefu wa Eneo la kufanyia  mazoezi na Television ya mkoa ya kuonyesha kazi zao. 
" Tunatamani kupata eneo la kufanyia shughuli zetu hususani mazoezi kwani tulizoea kufanyia shule ya msingi makubusho ambapo kwa sasa tumefukuzwa , hatuna  sehemu ya Uhuru kufanyia mazoezi yetu" alisema Chalo. 
Alisema walikuwa wamepanga kujenga Meru Village sehemu ambapo wangepata uwanja mpana wa kufanyia mazoezi lakini hadi sasa hawajafanikiwa kutokana na kukosa sapoti. 
"Kama vile wasanii wa Dar es salam walivyopatiwa eneo kule Bagamoyo na sisi tunapenda  tukumbukwe  katika hili ili tuwe huru  katika kufanya shughuli zetu pamoja na pia tuweze kutambulika" alisema. 
Aliwataka wana Arusha kununua kazi za wasanii wa Arusha na wasiegemee tu upande mmoja wa filamu za Kikorea ( seasons) wakawasahau watu wa nyumbani jambo linalorudisha nyuma maendeleo ya wasanii Arusha na Tanzania kwa ujumla. 
Naye Mmoja wa wasanii hao Experinsia Musa akisoma risala mbele ya Mkuu wa mkoa alisema pamoja na kupatiwa  eneo la kujenga ofisi zao, bado wanakabiliwa na eneo la kilimo na ufugaji kwa wale wasanii wasiokuwa na ajira ili waweze kujiajiri kupitia kilimo na ufugaji. 
 Mwenyekiti wa Shirikisho la waigizaji wa filamu jijini Arusha(TDFAA) Isack Chalo akiwa anaimba moja ya nyimbo zake alizozirekodi 
 wasanii walionyesha ujuzi wa aina mbalimbali kila mtu na kipaji  
 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiongea na wasanii wa mkoa wa Arusha waliouthuria semina ya Ujasiriamali iliyofanyika leo katika viwanja vya shule ya msingi ya Arusha School iliopo jijini hapa 
 wasanii wa aina mbalimbali wakiwa wanamsikiliza mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwa makini 
 Kaimu Afisa maendeleo ya Jamii Jiji Tajieli Mahega akiwa anasoma risala fupi inayoelezea lengo la kuandaa mafunzo hayo kwa wasanii hao 
 Kaimu mkurugenzi wa jiji la Arusha Rebeka  Mongi akiwa anaongea na wasanii wa mkoa wa Arusha waliouthuria mafunzo hayo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Arusha 
 Wasanii wa mkoa wa Arusha pia waliatumia fursa hiyo kumkabidhi mkuu wa mkoa huu Mrisho Gambo baadhi ya kazi zao ambazo wamezifanya ili nayeye azione na aweze kuwasadia zaidi 
 kila mmoja alionyesha kipaji chake msanii huyu alionyesha kipaji cha kuimba 
 Mwenyekiti wa Shirikisho la waigizaji wa filamu jijini Arusha(TDFAA) Isack Chalo akiwa anaimba moja ya nyimbo zake alizozirekodi 
 wasanii walionyesha ujuzi wa aina mbalimbali kila mtu na kipaji chake 
 | 

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni