MIILI YA WATU 162 IMEPATIKANA HADI SASA BAADA YA BOTI ILIYOBEBA WAHAMIAJI KUZAMA MISRI

Idadi ya miili iliyopatikana baada ya boti ya wahamiaji kuzama katika pwani ya Misri siku ya jumatano, imefikia watu 162, huku zoezi la kutafuta miili zaidi likiendelea.

Boti hiyo ilikuwa imebeba wahamiaji kati ya 450 hadi 600 wakati ilipozama kilomita 12 kutoka bandari ya Rosetta.
Boti hiyo ilikuwa ikisafirisha wahamiaji kutoka nchi za Misri, Syria, Sudani, Eritrea pamoja na Somalia. Watu 163 tu ndio inasemekana wameokolewa.
                        Wahamiaji walionusuriwa katika boti iliyozama wakiwa taabani

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni