MTUHUMIWA WA MABOMU JIJINI NEW YORK NA NEW JERSEY ATIWA NGUVUNI

Mtuhumiwa wa mabomu ya Jijini New York na New Jersey anashikiliwa na polisi baada ya kurushiana risasi na polisi baada ya kukutwa amelala kwenye mlango wa baa.

Mtuhumiwa huyo Ahmad Khan Rahami, 28, anafanyiwa upasuaji wa kwenye jeraha la risasi. Maafisa polisi wawili nao wamejeruhiwa katika tukio hilo huko Linden, New Jersey.

Meya wa Linden Derek Armstead amesema kuwa mmiliki wa baa alimkuta mtuhumiwa huyo akiwa kwenye mlango wa baa yake na kuripoti polisi.
Mtuhumiwa wa milipuko ya mabomu New York na New Jersey akiwa kalala chini huku amefungwa pingu kwa nyuma 
Mtuhumiwa ya milipuko ya mabomu ya New York na New Jersey akiingizwa kwenye gari la wagonjwa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni