Mkuu wa wialaya Mh Richard Kasesela akitoa hotuba wakati wa maonesho ya wajasiliamali aliyoyaandaa katika barabara ya Olofea Manispaa ya Iringa.
Mkuu wa
mkoa wa Iringa Mh. Amina Masenza amefungua maonesho ya wajasiliamali
yalioandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela katika
barabara ya Olofea Manispaa ya Iringa.
Akifungu
Maonyesho hayo, aliwaasa wana vikundi kuwa na umoja ili kufanikisha
ndoto zao. Pia aliagiza benki ya Posta kuhakikisha wanawasaidia mikopo
wajasiliamali hayo.
Mapema
akimkaribisha Mkuu wa mkoa , Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard
Kasesela alimshukuru Mkuu wa mkoa kwa kukubali kuwa mgeni rasmi na
kumuomba maonesho hayo yawe yanafanyika mara kwa mara ili wajasiliamali
wapate soko na kujikwamua kwa uchumi.
Meneja wa
Benki ya Posta Mkoa wa Iringa Bwana Kayanda aliwambia wajasiliamali
pesa ipo, ila wakopaji ndio hakuna hivyo anawakaribisha waje kukopa.
Zaidi ya
wajasiliamali 600 walipata mafunzo yaliyoandaliwa na Mh Kasesela hapo
tarehe 18/8/16, na leo ilikuwa siku ya kuonyesha bidhaa hizo.
Pia kilikuwepo kikundi ambacho kinatengeneza mipira ya kuchezea mpira wa miguu cha kata ya Ruaha.
Mkuu wa mkoa Bi Amina Msenza akipata maelezo kutoka kwa wajasiliamali baada ya ufunguzi wa amonyesho hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni