Na  Mwandishi Maalum,
New York
Shirika lisilo la 
Kiserikali    la
Speak 
Up for Afrika    limemtunukia tuzo, Rais Mstaafu Jakaya Mrisho
Kikwete kutokana na uongozi wake wa kisiasa na utetezi wake  kwa  makundi ya jamii yaliyo katika mazingira magumu
hususani wanawake na watoto.
Utoaji wa  Tuzo hiyo  ya 
uongozi wa kisiasa na utetezi , umekwenda sambamba na   hafla ya 
miaka mitano ya kuanzishwa kwa  Taasisi ya Speak up  Afrika. Hafla  hiyo iliyofanyika jana Alhamisi Jijini New
York   ilikuwa  pia  ni
sehemu ya kuhamasisha uchangiaji   wa shughuli za 
Taasisi hiyo.
Mchango
 ambao umetambuliwa na 
Speak Up  Afrika,   taasisi ambayo imekuwa ikifanya kazi  kwa Karibu na 
Rais Mstaafu Kikwete, ni  katika maeneo ya  upelekaji na usambazaji wa 
huduma za msingi
za afya hususani afya ya mama na mtoto, 
udhibiti wa  ugonjwa  wa malaria kupitia kampeni  ya malaria haikubaliki
 ,usambazaji wa
vyandarua  vyenye viatilifu, kampeni
ya  lishe bora, na  kampeni ya  
chanjo kwa watoto. 
Pamoja 
 na  kutambua 
juhudi za   Rais Mstaafu  Kikwete katika  kuyasemea maeneo hayo,  
Taasisi hiyo kupitia  Mkurugenzi wake  Mtendaji Bi. Kate Campana pia 
imemtambua  kama kiongozi ambaye    amekuwa mstari wa mbele  wa kulisema
 Bara la Afrika kila  mara alipopata  fursa 
ya  kufanya hivyo wakati akiwa
madarakani na hata baada ya kustaafu.
Rais kikwete ameelezwa katika hafla hiyo
iliyowashirikisha  wadau wa kada
mbalimbali, kama kiongozi wa kisiasa ambaye amezigusa nyoyo za watu wengi
kujitolea kwaajili ya watu wenye mahitajio ya kupata huduma za msingi za
kijamii ambazo  au wameshindwa kuzipata
kutokana na kipato kidogo au haziwafikii kabisa.
Akipokea  Tuzo hiyo,
Rais  Mstaafu Kikwete , amesema Tuzo hiyo
ni ya watoto wote  waafrika ambao
ndio  waliomfanya asimame   mbele
ya wageni waalik
“
 Ni kwa sababu yenu ndio sababu nimetenga muda wangu  baada ya kustaafu 
kusukuma mbele agenda
ya  kuboresha maisha yanu. Ninafanya
hivyo kwasababu makuzi yangu yalikuwa kama  ya mtoto yeyote yule wa  
kiafrika, nimeyaishi maisha  wanayo ishi. Na kwa hiyo ninaelewa fika 
 hamu na kiu yao ya kuwa  na maisha bora na afya njema”. Akasema
Kikwete na kushangiliwa na wageni waalikwa.
Akaongeza
 kuwa  ,  mafaniko ambayo ameyapata katika  juhudi hizo  za kufikisha 
huduma za msingi  za kijamii kwa makundi  yenye mahitaji  yametokana na 
mambo mawili makubwa moja
ni   aina ya uongozi  alioutumia kusukuma harakati hizo. Na pili 
 uhamasishaji uliofanyika katika  kupiga vita malaria kupitia Speak Up 
Afrika na
   kampeni yao ya  malaria haikubaliki.
“ Nisingeweza kuyafanya niliyoyafanya   bila uungugwaji mkono na  ushirikiano 
wa karibu nilioupata  na ninaoupata
kutoka taasisi za kimataifa  ikiwamo hii
ya  Speak Up  Afrika. Ndio maana  kwa mfano, 
tumeweza kupunguza visa vya malaria kwa  
theluthi mbilli, 
tumefanikisha  upatikanaji wa
chanjo kwa asilimia 96 kwa watoto wote na kupunguza vifo vitokanavyo na  malaria kwa 
 nusu.” Akaeleza Kikwete na
kushangiliwa  tena.
Akasema,
 anamini katika ushirikiano na wadau mbalimbali  kama akina Ray Chambers
 kupitia kampeni
ya  hakuna tena malaria, Taasisi ya  Bili na Melinda Gates na Gavi 
Vaccination   Alliance ambayo anashirikiano  nayo kwa karibu katika  
kampeni ya chanjo kwa wote.
Rais  Mstaafu
amewahakikishia   watendaji wa Speak  Up Afrika kwamba  ataendelea kufanya kazi nao kwa karibu  kutokana 
kile alichosema amejionea mwenye kazi nzuri wanayoifana.
 Akawasihi 
 wadau mbalimbali  kuichangia taasisi hiyo  kwa kile alichosema, 
inafanya kazi kubwa  ya siyo tu kufikisha huduma za kijamii pale
zinapotakiwa lakini  pia imekuwa ni
kipaza sauti cha Afrika.
Wengine waliopewa Tuzo kwa kutambua michango yao kwa jamii
ni  pamoja na   Professa Awa Marie Coll- Seck, Waziri wa
Afya  wa Senegal, Bibi Toyin  Saraki, 
mwanzilishi wa Taasisi ya 
Wellbeing  Afrika ambayo  pia imekuwa ikitoa  elimu na misaada kwa wanawake na watoto
pamoja na elimu  kwa wakunga na kutambua
kazi nzuri, kubwa na ngumu  ya
kuwahudumia wanawake wenzao wanapojifungua. 
Na  Bwana Kabirou Mbodje ambaye ni
Mkurugenzi mtendaji wa  Taasisi ya  Wari. 
Taasisi ya  Speak  Up 
Afrika  imeanzishwa  na wanawake na inaongozwa na wanawake. Ni
taasisi ambayo imejijengea uweo na sifa kubwa ndani  ya kipindi cha miaka mitano tangu  kuanzishwa kwake.   

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni