Naibu
 Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. 
Suzan Kolimba (katikati), akizungumza na madereva 10 wa Tanzania 
waliotekwa na watu wanaodaiwa kuwa ni waasi Jamhuri ya Demokrasia ya 
Conco (DRC), wakati wa hafla fupi ya kuwapokea iliyofanyika Uwanja wa 
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo jioni. Kulia ni 
Balozi wa Congo nchini, Jean Mutamba na kushoto ni Mkurugenzi  Idara ya Afrika katika wizara hiyo, Balozi Samweli Shelukindo.
 Balozi wa Congo nchini, Jean Mutamba (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo.
 Mmiliki
 wa Kampuni ya Simba Logistic ambayo magari yake na madereva walitekwa, 
Azim Dewj (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo ya kuwapokea madereva
 hao.
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakisubiri kuchukua taarifa za kuwapokea madereva hao.
 Madereva hao wakipokelewa uwanjani hapo.
 Madereva hao wakiwa chumba cha mkutano cha uwanja huo wakati wa mapokezi yao.
Dereva  Mbwana Said (kulia), akielezea jinsi walivyotekwa.
 Dereva Kumbuka Seleman (kulia), akisimulia jinsi alivyotoroka na kutoa taarifa ya kutekwa kwao.
Dereva
  Athuman Fadhili (kulia), akisimulia walivyookolewa na majeshi ya Congo
 na jinsi walivyojificha porini na kutembea umbali mrefu kwa kutambaa 
ambapo ilifika wakati waliomba bora wafe kuliko mateso waliyokuwa 
wakipata.
 Hapa ni furaha ya kukutana na ndugu jamaa na wafanyakazi wenzao.
 Picha ya pamoja na viongozi waliowapokea.
 Ndugu, Jamaa, marafiki na wafanyakazi wenzao wakiwa nje ya jengo la VIP uwanjani hapo wakisubiri kuwapokea.
 Mapokezi yakiendelea.
Ni furaha ya kukutana na wapendwa wao.
Hapa Dereva Mbwana Said akikumbatia na mjomba wake Kassim Salim katika hafla hiyo kwa Mbwana ilikuwa ni furaha na majonzi. 
Mbwana Said (katikati), haamini macho yake baada ya kukutana na mke wake Mariam pamoja na mtoto wake Kauzari.
Na Dotto Mwaibale
MADEREVA
 10 wa Tanzania waliotekwa na watu  wanaodhaniwa ni waasi Jamhuri ya 
Demokraia ya Congo (DRC) wamesema waliponea tundu la sindano kuuawa.
Kauli 
hiyo imetolewa na madereva hao katika hafla ya kuwapokelewa iliyofanyika
 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo
 jioni.
Akizungumza
 kwa niaba ya wenzake Mbwana Said alisema analishukuru jeshi la Congo 
kwa jitihada kubwa walioifanya kwa ajili ya kuokoa maisha yao." 
" 
Tunaishukuru serikali ya Congo kwa kutuokoa kwani tulikuwa katika wakati
 mgumu na leo kuungana tena na ndugu zetu" alisema Said.
Alisema
 walilazimia kutembea kwa muda mrefu huku risasi zikirindima kati ya 
majeshi ya serikali na waasi hao hadi walipofanikiwa kutuokowa kutoka 
kwenye mikono ya waasi hao. 
Naibu 
Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. 
Suzan Kolimba aliishukuru serikali ya Congo kwa jitihada iliyoifanya na 
kufanikiwa kuwaokoa madereva hao.
Balozi
 wa Congo nchini Jean Mutamba aliwataka madereva hao kuacha viza na 
nyaraka zao ubalozini pindi wanapo safiri na kurudi ili iwe rahisi 
kuwatambua pale wanapopata matatizo.
"Tukio hilo limetokea kwa bahati mbaya na kutoa wito kuwa waendelee kusafiri kwa kufuata taratibu zilizopo," alisema Mutamba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni