JUMLA YA WATOTO 4000 WANAZALIWA NA TATIZO LA KICHWA KIKUBWA NA MGONGO WAZI KILA MWAKA HAPA NCHINI TANZANIA


 


 Kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr.Othman  Kiloloma akimuonyesha mkuu wa wilaya  ya Arusha
Gabriel Daqarro sehemu ambayo mtoto amefanyiwa upasuaji wa kichwa
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akiwasili katika hospitali ya Mount Meru iliopo jijini hapa Tayari kwakwenda kuangalia watoto waliofanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa
  Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini akimkabidhi pampas moja ya mama mzazi wa mtoto ambaye amefanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa ikiwa ni moja ya zawadi walizopatiwa na GSM Foundation
Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqarro akielekea kwenye wodi akiongozwa na dkta  mkuu wa mkoa wa Arusha Frida mokiti naKaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr.Othman Kiloloma 
Kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr.Othman Kiloloma akiwa anampa mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro maelekezo ya picha inayoonyesha jinsi mtoto alivyokuwa kabla ya kufanyiwa upasuaji
  Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea watoto waliofanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa kikubwa
                                                          

                                                           
                                                         Na Mahmoud Ahmad, Arusha

Jumla ya watoto 4000 wanazaliwa kila mwaka na tatizo la kichwa kikubwa na mgongo wazi na kati ya hao ni watoto 500 tu ndio wanafikishwa hospitalini kwa ajili ya upasuaji huku wengine 3500 awajulikani wanapopelekwa.

Hayo yamebainishwa leo na kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr.Othman Kiloloma wakati akiongea na waandishi Wa Habari Mkoani hapa.

Alisema kuwa wao kama taasisi ya moi walikaachini na kuona kunawatoto wengi ambao wanazaliwa na vichwa vikubwa lakini hawafiki hospitalini kwa ajili ya garama huku wengine wakiwa wanaamini imani za kishirikina kitu ambacho sivyo.

Alibainisha kuwa mpaka sasa wameshatembelea mikoa 13 ambayo ni awamu ya kwanza na wameshafanya upasuaji jumla ya watoto 167 ambapo kwa mkoa Wa Arusha wamewaona watoto 35 na wamewafanyia upasuaji watoto sita.

"Kila mwaka watoto 4000 wanazaliwa na kati yao 500 tu ndio wanafikishwa hospitali lakini watoto wanaobaki 35000 atujui wanaenda wapi au wanapelekwa wapi maana hospitalini awaji"alisema Kiloloma

Kwa upande wao wagonjwa waliofanyiwa upasuaji Wa kichwa Nasson Daniel 17 aliyelazwa katika wodi ya majeruhi wanaume no 3 pamoja na Aisha Amir Suleiman 17aliyelazwa wodi ya majeruhi wanawake wameiomba jamii wasiwafiche watoto wenye matatizo ndani wawatoe ili wakatibiwe kama walivyotibiwa wao.

Akizungumza kwa niaba ya wazazi wenye watoto waliofanyiwa upasuaji Emelda Buxay (36)amesema kuwa amewaomba huduma hii isogezwe karibu na jamii maana watoto wengi wenye matatizo kama haya wapo vijijini wanateseka na hawana msaada .

"Wazazi wenzangu haswa wakina mama sisi ndiyo tunakaa na watoto kwa mud a mrefu ndiyo tunaweza kugundua mabadiliko ya mtoto ,tusisikilize dhihaka za watu mtaani ambazo Mara nyingi watu wamekuwa wakisema pale wanapoona mtoto mwenye ulemavu wowote hebu tuchukue hatua tuwapeleke hospitalini,kama vile mtoto wangu Dorcus alivyofanyiwa upasuaji leo ni Siku ya tatu kichwa kinaendelea kupungua ,tusiwafiche watoto jamani "alisisitiza Emelda.

Naye mkuu Wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro alitoa wito kwa jamii hususa ni wazazi kutowaficha watoto wenye tatizo hilo kwani tatizo linatibika na mtoto anapona kabisa .

Alisema anapenda kuwashukuru madaktari hawa walioibua na kuangalia namna gani wanaweza kusaidia watoto hawa pamoja na shirika la GSM foundation ambao ndio waliothamini Huduma hii ya upasuaji bure ambapo alisema kwa upande wa Arusha jumla ya watoto 35 wameonwa huku watoto sita wakiwa wamekishwa fanyiwa upasuaji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni