Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikata tiketi
ya mabasi ya Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT katika Kituo cha
Ubungo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusafiri na mabasi hayo kutoka
katika kituo hicho kuelekea Posta. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama
Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga naye akiwa mmoja wa
wasafiri wa mabasi hayo. Masauni aliyapanda basi la Mwendo kasi mara
baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo
kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Picha zote na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiigusisha
tiketi yake katika mashine ya Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT
katika Kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam ili mruhusu kuingia ndani
ya stendi hiyo kwa ajili ya kusafiri na mabasi hayo kutoka katika kituo
hicho kuelekea Posta. Mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika
Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa
abiria Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiingia ndani
ya Basi la Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT katika Kituo cha
Ubungo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusafiri na basi hilo kuelekea
katikati ya Jiji, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu
ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa ndani
ya moja ya mabasi ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi ya UDA-RT jijini Dar
es Salaam akitoka kituo cha Ubungo kuelekea katikati ya Jiji, baada ya
kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua
mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitelemka
katika moja ya mabasi ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi ya UDA-RT jijini
Dar es Salaam katika kituo cha Nyerere, Posta. Masauni alipanda basi
hilo akitokea Ubungo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi
Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiondoka
katika Kituo cha Mabasi ya Mwendokasi cha Nyerere, Posta, mara baada ya
kusafiri na usafiri huo akitokea Ubungo, jijini Dar es Salaam, baada ya
kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua
mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Katikati ni Mkuu wa Kikosi
cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga Picha zote
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Felix Mwagara, MOHA
NAIBU
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameupongeza
Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT wa jijini Dar es Salaam na
kuwataka wananchi waendelee kuyatumia mabasi hayo wanaposafiri sehemu
mbalimbali jijini humo.
Mhandisi Masauni ameyasema hayo jana
mara baada ya kusafiri na mabasi hayo kutoka kituo cha mabasi hayo cha
Ubungo mpaka katikati ya jiji kwa lengo la kujionea jinsi mabasi hayo ya
mwendokasi yanavyohudumia abiria pamoja na kuwapa moyo wananchi kuwa
usafiri huo unatumiwa na mwananchi wa aina yeyote.
Akizungumzia
usafiri huo, Masauni alisema mradi huo umerahisisha sana usafiri kwani
ametumia dakika chake akitokea Ubungo hadi Posta katikati ya jiji bila
usumbufu wowote, hivyo mradi huo ameomba uendelee kulindwa pamoja na
kutunzwa na UDA-RT na wananchi wenyewe kwa ujumla.
“Mimi kwa
kweli nimeufurahia sana usafiri huu, Serikali imefanya jambo kubwa sana
kwa wananchi wake, kwa kuwajali wananchi kwa kuuleta mradi huu ambao
unarahisisha safari kwa uharaka zaidi na pia unapendezesha jiji kwa
jinsi magari yalivyo nadhifu,” alisema Masauni ambaye pia alilipa nauli
kwa kupanga foleni kama wananchi wengine wanavyofanya wanapotaka
kusafiri na usafiri huo.
Masauni aliongeza kuwa; “Nimefarijika
sana na lugha ya adabu na tulivu ambayo wanaitumia madereva wa mabasi
hayo wanapowatangazia wananchi vituo mbalimbali vya kushuka na kuingia
kwenye mabasi hayo, hii inasaidia kuwa na mawasiliano mazuri na abiria,
pia inaonesha madereva hao wamefunzwa vizuri na wanaipenda kazi yao.”
Hata
hivyo, Masauni alitoa ushauri kwa uongozi wa mabasi hayo, kuruhusu
wananchi waingie ndani ya mabasi hayo kwa idadi ambayo haitaleta kero
kwa abiria wengine ili kupunguza wingi wa abiria hao kwa lengo la
kuepuka mbanano mkubwa wa abiria.
Pia aliwataka wananchi wa jiji
hilo kuyatunza mabasi hayo, na pia kukubali maelekezo ya madereva
wanapotoa matangazo wanapokuwa safarini kuelekea maeneo mbalimbali ya
jiji.
Naibu Waziri huyo alipanda mabasi hayo akitokea Ubungo
mara baada ya kumaliza ziara yake ya kushtukiza kwa kutembelea Stendi
Kuu ya Mabasi Ubungo kwa lengo la kukagua mabasi mabovu pamoja na
usalama wa abiria wanaosafiri na mabasi hayo. Masauni pia alifanya
ziara hiyo ya ghafla kwa kutembelea Stendi ya Kibaha, mkoani Pwani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni