Mmoja wa makocha wanaoheshimika sana Afrika Mashariki, ambaye pia aliwahikuwa mchezaji mkubwa wa soka James Siang’a amefariki dunia jana huko Bungoma nchini Kenya baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa afisa wa chama cha Kefoca, Bob Oyugi, Siang’a ambaye aliwahi kuchezea Gor Mahia, Luo Union na timu ya taifa Kenya Harambee Stars kama kipa amefariki dunia majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo.
Mbali na kuichezea Harambe Stars Siang’a pia alikuwa kocha wa Harambee Stara katika mwaka 1999 hadi 2000, kisha kuja Tanzania kuinoa Taifa Stars mwaka 2002. Pia aliwahi kuwa kocha wa klabu za Simba, Moro United na Express ya Uganda.

Akiwa na Moro United Oktoba 2004 Siang’a aliombwa kuinoa Taifa Stars lakini alikataa. Siang’a pia aliinoa Mtibwa Sugar kabla ya kurejea Kenya kuifundisha timu ya Gor Mahia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni