Baraza
la madiwani Halmashauri ya Monduli limewafukuza kazi watumishi wawili
na wawili kupewa onyo kali huku baraza hilo likiridhia mwanasheria wa
Halmashauri hiyo kurejea kazini baada ya kushinda kesi
Akiwataja watumishi hao Mwenyakiti wa baraza la madiwani
isack Joseph Kopriano ameeleza kuwa wamejadiliana kwamuda mrefu
kuhusiana na watumishi hao na ndipo wakafikia maamuzi ya kuwafukuza kazi
Mrasimu ramani Leonard Mkwave pamoja na Afisa ardhi mteule
Kitundu Mkumbo,waliopewa.baraua za onyo ni Mkuu wa idara ya
ardhi ndugu Adili Mwanga pamoja na Afisa ardhi mpimaji Leonard Haule
huku baraza hilo likiridhia mkuu wa kitengo cha sheria Gidion Kamara
akirudishwa kazini baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili.
Hatua hiyo imetokana watumishi waliofukuzwa kazi baada ya
kukutwa na makosa mawili kila mmoja hali iliyopelekea baraza kuchukua
uamuzi wa kuwafuta kazi,ambapo wenzao wawili makosa yao hao walipewa
onyo kali.
Kwa upande wa mwanasheria alifikishwa mahakamani na
Takukuru lakini aliweza kushinda kesi hiyo na kukosa kuwa na tuhuma
ambazo zilizokuwa zinamkabili hivyo bataza likaridhia kumrudisha kazini.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri hiyo Stephen
Ulaya amesema kuwa atayafanyia kazi maagizo aliyopewa na mkuu wa wilaya
bila kumuonea mtu aibu wala kumpendelea wala kumuonea mtu na ataongoza
halmashauri kwa kufuata kanuni na taratibu.
Aidha Mkurugenzi huyo amewataka watumishi hususani watendaji wa vijiji na
kata kuhakikisha wanafuata taratibu na kanuni kwa kuitisha mikutano ya wananchi kwa wakati na yeyote atakayebainika kwenda kinyume na hilo sheria itafuata mkondo wake.
kata kuhakikisha wanafuata taratibu na kanuni kwa kuitisha mikutano ya wananchi kwa wakati na yeyote atakayebainika kwenda kinyume na hilo sheria itafuata mkondo wake.
Hata hivyo amewataka madiwani kuwapa ushirikiano watumishi
hao vitongoji vijiji na kata ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa mazowea
ili kuhakikisha wananchi wanapata hudumakwa wakati na kutoa michango yao
kwaajili ya maendeleo ya wilaya hiyo.
"Monduli ni yetu sote lazima tufanye kazi kwa bidii
kuhakikisha wananchi wanapata hudumakwa wakati, na sintamuonea haya mtu
wala aibu,mtumishi yeyote atakayekiuka sheria za utumishi ,ili
kuhakikisha maendeleo.yanawafikia wananchi kwa wakati, alisisitiza
ulaya"
Alibainisha kuwa yeyote atakayekutwa miradi yamaendeleo ipo
chini yakiwango na wanango na amabaye hatafanya mkutano mkuu wa wa
wananchi katika kitongoji,kikijina kata kwa wakati hatakuwa amejiondoa
mwenyewe.
Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Monduli Isack Joseph Kapriano.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Monduli Stephen Ulaya akiwa katika kikao cha baraza
la madiwani kilichofanyika kwa siku mbili wilayani humo.
Madiwani
wa Halmashauri ya Monduli wakiwa katika kikao cha pamoja kujadili
maendeleo ya kata zao na changamoto mbalimbali za wananchi.
Watumishi
wa Halmashauri ya Monduli pamoja na Wataalamu pia walihudhuria katika
Baraza hilo la madiwani lililofanyika kwa siku mbili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni