Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akiwa ameambatana pamoja na
wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Geita, jana wakati
alipotembea ofisi za Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali (Mst) Ezekiel
E. Kyunga (watatu kutoka kushoto), IGP Mangu yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya kipolisi.
Mkuu
wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali (Mst) Ezekiel E. Kyunga, akitoa neno la
ukaribisho kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, ambaye
yupo katika ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya kipolisi,
anayefuata ni kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, SACP Mponjoli Mwabulambo.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akifuatilia jambo kwa
makini kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali (Mst) Ezekiel E.
Kyunga, pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani humo
jana akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya kipolisi.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akitoa neno mbele ya kamati
ya ulinzi na usalama mkoa wa Geita, jana wakati akiwa katika ziara ya
kikazi ya kukagua miundombinu ya kipolisi.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akiweka sahihi katika
kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya
Chato mkoani Geita, kwa ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya
kipolisi mkoani humo, katikati ni Mkuu wa wilaya ya Chato, Mhe. Shaaban
Ntarambe, akifuatiwa na kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, SACP Mponjoli
Mwabulambo.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, pamoja na timu ya maofisa
na kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, SACP Mponjoli Mwabulambo,
wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa wilaya ya Chato, Mhe. Shaaban
Ntarambe, alipomtembelea ofisini kwake jana wakati akiwa katika ziara ya
kikazi ya kukagua miundombinu ya kipolisi.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akiwa katika kituo kikuu
cha Polisi wilaya ya Chato mkoani Geita, jana alipotembelea kituo hicho
wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya
kipolisi. (Picha zote na Demetrius Njimbwi - Jeshi la Polisi)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni