Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminieli Aligaesha
(kushoto) kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akipokea msaada wa
seti ya televisheni yenye thamani ya Sh 2.4 milioni kwa ajili ya jengo
la wazazi (Maternity II). Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana
wa Kibosho (UVIKI), Severine Mushi akikabidhi msaada huo LEO na
anayefuatia ni Mwenyekiti wa UVIKI, Marcel Mushi (wa tatu kushoto).
Mlezi
wa umoja huo, Dk Methew Kalanga ambaye ni Mkuu wa Idara ya Kinamama
Muhimbili akiwapongeza vijana hao kwa kutoa msaada wa seti ya
televisheni na kuchagia damu leo. Kulia ni Kaimu Meneja wa Jengo la
Wazazi namba mbili, Sister Stella Gerald.
Vijana wa umoja hao wakimsikiliza Dk Kalanga baada ya hospitali hiyo kupokea msaada wa seti ya televisheni leo.
Vijana hao wakipewa maelezo na Ofisa Ustawi, Ndekusara Makishe kabla ya kuchangia damu leo.
Vijana hao wakichangia damu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
Mercy Kaanaeli, MNH.
HOSPITALI
ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea jumla uniti 19 za damu kutoka
kikundi cha Umoja wa Vijana wa Kibosho (UVIKI). Kikundi hicho chenye
wanachama 40 kimeka katika hospitali hiyo leo na kutoa msaada wa seti ya
televisheni na kuchangia damu.
Msaada
huo umetolewa leo katika hospitali hiyo una thamani ya Sh 2.4 milioni
na seti hiyo itafungwa katika Jengo la wazazi namba mbili. Seti hiyo
inahusisha Runinga moja ya nchi 50, Dishi na King’amuzi cha AZAM pamoja
na deki.
Akishukuru
baada ya kupokea seti hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma
kwa Wateja, Aminieli Aligaesha amesema seti hiyo ya televisheni
itatumika kutoa elimu ya afya kwa kinamama wajawazito.
Kaimu
Meneja wa Jengo la Wazazi namba mbili, Stella Gerald amesema seti hiyo
ni msaada mkubwa na kwamba itasaidia kuelimisha kina mama wakati
wakisubiri kupata huduma.
“Huwa
tunatoa elimu ya maandalizi kwa kinamama ikiwamo vidokezo vya hatari,
uandaaji wa chakula lishe pamoja na mambo yanayopaswa kufanywa, hivyo
badala ya muuguzi kuongea tutatumia runinga kutoa elimu hiyo,”amesema
Stella.
Naye
Mkuu wa Idara ya Kinamama, Dk Matthew Kallanga amesema mchango wa damu
uliotolewa na kikundi hicho utasaidia kina mama kuwa na uzazi salama.
“Damu
iliyochangiwa na kikundi hiki, itasaidia kina mama kuwa na uzazi salama
kwani mama mjamzito mmoja huweza kutumia chupa 5 hadi 6,” amesema.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminieli Aligaesha
ametoa wito kwa jamii kuiga mfano wa kikundi cha UVIKI na kutoa damu kwa
wingi ili kuokoa maisha ya wagonjwa.
Mwenyekiti
wa Kikundi cha UVIKI, Marcel Mushi amesema kuwa watatoa elimu katika
jamii wanayoishi ili wanajamii wengi zaidi wajitokeze kuchangia damu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni