KIFAA KINACHOTILIWA SHAKA CHALIPUKA NEWS JERSY NCHINI MAREKANI


Kifaa kinachotiliwa shaka kilichokutwa karibu na reli Mjini New Jersey kimelipuka wakati wataalam wa mabomu wakijaribu kukizima kwa kutumia roboti.

Kifaa hicho ni miongoni mwa vitano vilivyopatikana kwenye begi la mgongoni lililotupwa kwenye takataka karibu na Elizabeth, kwa mujibu wa meya wa Jiji hilo.

Kubainika kwa vifaa hivyo vya milipuko kunafuatia shambulizi la mwishoni mwa wiki la mabomu Jijini New York na New Jersey na tukio la shambulizi la kisu huko Minnesota. 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni