Mbunge Bonnah Kaluwa Achangisha Milioni 13.7 Ujenzi Kituo cha Yatima.


Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa akinadi vitu mbalimbali katika harambee hiyo kuchangisha fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre Victorius (CVC), chini ya Mchungaji Jehu Mkono.Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa akizungumza katika harambee hiyo kuchangisha fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre Victorius (CVC), chini ya Mchungaji Jehu Mkono.

 MBUNGE wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa ameongoza harambee ya uchangishaji wa fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre Victorius (CVC), chini ya Mchungaji Jehu Mkono. Harambee hiyo ilifanyika katika Kanisa la Deliverance Centre Victorius Tegeta kwa Ndevu, jijini Dar es Salaam, ambapo Bonnah Kaluwa alikuwa mgeni rasmi na kufanikiwa kukusanya fedha shilingi 13,730,000 ambazo zilipatikana kwa michango ya waumini, wageni waalikwa na kufanyika kwa mnada ulionadi vitu anuai.

 Katika harambee hizo Mbunge, Kaluwa alitoa shilingi milioni mbili yeye pamoja na mumewe huku akiendesha mnada uliotunisha mfuko wa ujenzi wa kituo hicho. Awali akizungumza katika harambee hiyo Mwenyekiti wa umoja wa akinamama wa kanisa la CVC, Rose Haji Mwalimu alisema harambee hiyo itawezesha kupatikana kwa fedha za ujenzi wa kituo pamoja na upanuzi wa kanisa la CVC eneo la Tegeta mradi unaotarajia kutumia shilingi milioni 40.
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa (wa tatu kulia) akikata keki kuashiria uzinduzi wa harambee hiyo iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre Victorius.Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa (wa pili kulia) akipeana mkono na Mwenyekiti wa umoja wa akinamama katika Kanisa la Deliverance Centre Victorius, Rose Haji Mwalimu (kulia) mara baada kukabidhi risala ya ujenzi wa kituo hicho. Kushoto ni Hoyce Temu, ambaye ni mwanakamati wa harambee hiyo.Meza kuu ikimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa (hayupo pichani akizungumza) katika harambee ya uchangishaji wa fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre Victorius (CVC).Askofu Fedrick Ndonde (kushoto) ambaye ni rafiki wa karibu wa Kiongozi Mkuu wa CVC Deliverance Centre Victorius, Mchungaji Jehu Mkono akizungumza katika hafla hiyo.Hoyce Temu (kushoto) ambaye ni mwanakamati wa harambee ya uchangishaji wa fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre Victorius (CVC) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa na mgeni rasmi katika hafla hiyo.Kiongozi Mkuu wa CVC Deliverance Centre Victorius, Mchungaji Jehu Mkono (kulia) akishusha maombi kabla ya kuanza kwa harambee hiyo ya uchangishaji wa fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta.Baadhi ya wageni waalikwa katika harambee iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre Victorius (CVC), chini ya Mchungaji Jehu Mkono wakiwa katika harambee hiyo.Mwimbaji wa muziki wa injili, Edson Mwasabwite (kulia) akitumbuiza katika hafla hiyo ya uchangishaji fedha huku akiungwa mkono na Mbunge, Bonnah Kaluwa na viongozi wengine.Baadhi ya waumini wa Kanisa la Deliverance Centre Victorius Tegeta kwa Ndevu, jijini Dar es Salaam, wakiwa katika harambee hiyo.Kutoka kushoto ni Askofu Fedrick Ndonde, mwanakamati wa harambee hiyo, Hoyce Temu pamoja na Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa wakiwa katika harambee hiyo.Kiongozi Mkuu wa CVC Deliverance Centre Victorius, Mchungaji Jehu Mkono (katikati) akiahidi kuchangia shilingi milioni moja katika mradi huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni