Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo
ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacqueline Mneney Maleko (wa tatu
kushoto) akiongozana na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa
pili kushoto) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya maonyesho ya 39
ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba', barabara ya Kilwa, jijini
Dar.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo
ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko (wa pili
kushoto) akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez wakati wakielekea katika banda la Shirika la Umoja wa Mataifa
lilipo Karume Hall mara tu baada ya kuwasili.
Na Modewjiblog team, Sabasaba
Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez,
akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea banda la Umoja wa
Mataifa leo katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara Sabasaba
amesema Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa miradi na
mikakati ya Umoja wa Mataifa miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki.
Ameongeza kuwa dunia sasa imekuwa kijiji
kimoja na Umoja wa Mataifa umekuwepo Tanzania hata kabla ya uhuru, hivyo
unakusudia kuendelea kuwepo kushirikiana na watanzania katika kutatua
matatizo kwenye Nyanja mbalimbali.
Bw. Alvaro amewataka watanzania
kusherehekea pamoja miaka 78 ya Umoja hapa nchini kwa kutoa maoni mbali
mbali na kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo.
Amesema kwa pamoja tunahitaji kuzungumzia
usawa wa kijinsia, masuala ya kisiasa, mabadiliko ya tabia nchi na mambo
ya kiuchumi kwa ajili ya ustawi wa taifa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko,
ameushukuru Umoja wa Mataifa kwa kufanya juhudi za kusaidia vijana
kuanzia ngazi za chini kabisa na kuwawezesha kuwa wajasiriamali.
Amesema kitendo cha Umoja huo kushiriki katika maonyesho ya Sabasaba sambamba na kijana Amos Mtambala waliyemuwezesha kwa kumpatia mafunzo ya sanaa za uchoraji kumeleta hamasa kubwa miongoni mwa vijana wasio na ajira nchini.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro
Rodriguez akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye banda
la Shirika la Umoja wa Mataifa katika viwanja vya maonyesho ya 39 ya
kimataifa ya biashara 'Sabasaba', barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo
ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko akisaini
kitabu cha wageni kwenye banda la Umoja wa Mataifa.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa
Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu, akitoa maelezo jinsi
wanavyoelimisha wananchi kuhusiana shughuli mbalimbali za Umoja wa
Mataifa nchini sambamba na malengo ya millenia yanayofikia kileleni kwa
Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyeambata na mwenyeji wake
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan
Trade), Jacqueline Mneney Maleko walipotembelea banda hilo kwenye
maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba', katika viwanja vya
Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa
Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akielezea maeneo ya Program
mbalimbali za UNDAP yaliyofanikiwa nchini Tanzania kwa Mratibu Mkazi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP)
nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) aliyeambata na mwenyeji wake
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan
Trade), Jacqueline Mneney Maleko.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa
Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akikabidhi taarifa ya mwaka
ya UNDAP kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko (katikati) aliyefuatana
na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) walipotembelea
banda la Shirika la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall.
Mkurugenzi na Meneja mradi wa TUBEGA
ART ambaye ni mtaalamu wa sanaa za uchoraji, Amos Mtambala, akitoa
maelezo jinsi alivyowezeshwa kupitia Shirika la Kazi Duniani (ILO)
kupata elimu inayomwezesha kuwa mjasiriamali kwa kuuza michoro hiyo
ndani ya banda la Umoja wa Mataifa kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez alipotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa
lililopo Karume Hall ndani ya viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya
kimataifa maarufu kama “Sabasaba”.
Afisa Mawasiliano wa Shirika la Kazi
Duniani (ILO) nchini, Magnus Minja akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kuhusiana na program ya kazi njenje ya
mradi wa kufundisha vijana katika shughuli za ujasiriamali inayoratibiwa
na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ambapo kijana Amos iliweze kumuinua na
kujiajiri kupitia sanaa ya uchoraji.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo
ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko, akionyesha
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya karatasi inayotoa
maelezo ya jinsi ya Watanzania wanavyoweza kushiriki kutoa maoni
mbalimbali juu ya utendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini
Tanzania kwa kutuma SMS ambayo ni bure bila malipo yoyote na moja kwa
moja kumfikia Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini Alvaro Rodriguez.
Jinsi ya kutuma ujumbe mfupi wa maandishi
(SMS), kwa kuandika neno UN au UMOJA WA MATAIFA ambapo kwa watumiaji wa
mtandao wa Airtel watatuma ujumbe wao kwenda namba 15453, kwa
watumiaji wa mtandao wa Tigo wanatuma kwenda 15055 au 15453 na kwa
Vodacom ni namba 15055.
Ambapo pia njia nyingine ya kuwasilisha maoni ya moja kwa moja ni kupitia mtandao wa (Online) kwa kubofya link hii http://gpl.cc/UN2
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo
ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko akizungumza
na waaandishi wa habari katika banda la Shirika la Umoja wa Mataifa
ambao wanashiriki maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba',
katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, vilivyopo barabara ya Kilwa, jijini
Dar. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro
Rodriguez akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya
Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko mfuko wenye
machapisho na vijarida mbalimbali vya Umoja wa Mataifa.
Afisa Utawala wa Wizara ya Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Suleiman Magoma (wa pili kushoto) akiuliza swali
kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) wakati
alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall katika
maonyesho ya Sabasaba. Kulia ni Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama na Wa pili kulia ni Mchumi
wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Vainess Molle.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro
Rodriguez akijibu swali la Bw. Suleiman.
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akionyesha namna ya kutoa
maoni ya utendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania kwa njia ya
SMS ambayo ni bure kwa mitandao yote ya simu za mkononi nchini kwa wadau
waliotembela banda la UN Tanzania.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro
Rodriguez ajibu maswali mbalimbali yalitumwa kwa njia ya mtandao na
wananchi katika banda la Umoja wa Mataifa maonyesho ya Sabasaba.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro
Rodriguez na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaotoa huduma katika banda la Umoja
wa Mataifa maonyesho ya Sabasaba.
Baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika picha ya pamoja na Mkuu wa UN Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni