Cheti cha ushindi wa Tatu ambacho Mbeya Yetu walikabidhiwa na TASO.
Hili ndilo Banda la Mbeya yetu Blog lililokuwa ndani ya Maonesho ya Nane nane Mbeya.
Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Blog na Mmoja wa wakurugenzi wa Tone Multimedia Company Limited Joseph Mwaisango kulia Akikabidhiwa Cheti cha ushindi wa tatu cha vyombo vya habari kikanda katika kurusha matukio yote ya Nane nane Jijini Mbeya na Mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Rajabu Mwambungu wa Pili Kushoto.
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Kilele cha Nane nane Kanda ya nyanda za juu Kusini Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Said Mwambungu wa pili kutoka kushoto aliye ongozana na Mbunge Mstaafu Dr. Chrisant Mzindakaya wa kwanza kutoka kulia pamoja na wageni wengine wakipata maelezo yakina ndani ya Banda la Mbeya yetu katika maonesho ya Nane nane. Mgeni Rasmi katika Maonesho ya Nane nane Kanda ya nyanda za juu Kusini Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Said Mwambungu wa Pili kutoka kushoto akipata maelekezo ya Kina kutoka kwa Mtaalam wa maswala ya Mitandao ya Kijamii Fredy Anthony Njeje wa kutoka Tone Multimedia Group Jinsi habari ambazo zipo katika Mtandano wa mbeya yetu zinavyoweza kupatikana pia kupitia simu ya Mkononi kiurahisi zaidi.
Mkuu wa Mkowa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro wa kwanza kulia akipata maelezo kutoka katika Banda la Mbeya ambapo alipata Taarifa fupi kuhusu Blog ya Mbeya yetu kutoka kwa Mtaalam wa Mitandao kutoka Tone Multimedia Group Fredy Anthony Njeje kwa Niaba ya Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango.
Mtoa Maelezo kutoka Tone Multimedia Group kupitia Mtandao wao wa Mbeya yetu Blog Fredy Anthony Njeje wa kwanza kulia akitoa maelezo ya kina kwa Mkuu wa Mkoa wa katavi Mh.Dr Rajab Lutengwe jinsi mtandao wa Mbeya yetu unavyofanya kazi pia unavyosaidia upatikanaji wa habari kwa urahisi kabisa. Pia kuekeza sababu za Kushiriki katika mashindano ya nane nane ikiwa ni pamoja na Kutoa elimu juu ya mitandao ya kijamii na faida zake hasa upande wa Blogs na matumizi sahihi.
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Mh. Mussa Zungiza wa kwanza kushoto akitoa neno la Pongezi kwa Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Blog Joseph Mwaisango kwa kazi nzuri ambayo inaendelea kufanyika kwa Blog ya Mbeya yetu.
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Mh Mussa Zungiza wa Kwanza kushoto akitoa pongezi kwa Tone Multimedia Group kwa kuwa wabunifu hasa walipo anzisha mkakati wa Blogs za Mikoa ambapo kila Mkoa unakuwa na habari yake, pia amesisitiza waandishi wengine na wamiliki wa mitandao ya Kijamii waige mfano kutoka hapa ili kuleta taarifa za uhakika na muhimu kwa jamii kwa ujumla. wa kwanza kutoka kulia ni Venance Matinya na Fredy Anthony Njeje.
Wa kwanza kushoto ni Rais wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa Habari Nchini Tanzania (UTPC) Kenny Simbaya alipotembelea Banda la Mbeya yetu na kujionea mambo mengi na Jinsi mtandao wa Mbeya yetu unavyofanya kazi.
Kutoka Kulia ni Mwandishi Mkuu wa Mbeya Yetu Blog na Msimamizi wa Mtandao huo ambao unamilikiwa na Tone Multimedia Group ambaye pia ni Mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni hiyo Joseph mwaisango, Gasper Kutoka Ebony FM, Ray Kutoka Ebony FM, Bony Kutoka Ebony FM na Fredy Anthony Njeje Kutoka Tone Multimedia Group .
Mwandishi Mkuu wa Mbeya Yetu Blog na Msimamizi wa Mtandao huo ambao unamilikiwa na Tone Multimedia Group ambaye pia ni Mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni hiyo Joseph mwaisango wa kwanza kushoto akitoa maelekezo kwa waliotembelea Banda la Mbeya yetu Blog, wa pili kutoka kushoto ni Mmiliki wa Mtandao wa Kajuna Son Blog Cathbert Angelo.
Wa kwanza kushoto ni Fredy Anthony Njeje kutoka Tone Multimedia , Cathbert Angelo Mmiliki wa Mtandao wa Kajuna Son Blog ambaye pia alikuja tembelea Banda la Mbeya yetu pamoja na Mpanji Mtangazaji wa Clouds Tv na Radio Mkoani Mbeya.
Chama Cha Wakulima Tanzania (TASO) kanda ya Nyanda za juu Kusini, kimeutunuku cheti mtandao wa kijamii wa www.mbeyayetu.blogspot.com ambao upo chini ya Tone Multimedia Company Limited kutokana na kuibuka mshindi wa TATU wa kurusha matangazo Kikanda katika maonesho ya Wakulima nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya John Mwakagale Uyole Jijini Mbeya.
Tuzo hiyo imekuja kutokana na kikosi cha Mtandao huu kuweka kambi katika maonesho hayo na kufanya shughuli za kurusha matangazo moja kwa moja kutoka uwanjani hapo na kuwapagawisha wakulima ambao walipata fursa ya kutembelea banda letu na kujionea habari zilizotokea muda huo huo na kuonekjana hewani.
Mbali na wakulima na watu mbali mbali waliokuwepo uwanjani hapo pia viongozi wa Taso na wakuu wa Mikoa pia walipata fursa ya kutembelea banda la Mtandao huu katika ziara zao za kukagua mabanda na hivyo kutoa sifa kwa wamiliki wa Mtandao huu namna habari zilivyokuwa zikienda kwa wakati.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh. Rajab Rutengwe ambaye ndiye alikiwa wa kwanza Kwanza kufanya ziara hiyo na kukuta habari zake tokea akipokelea mlangoni hadi kufikia mabanda habari zilikuwa hewani, aliupongeza mtandao wa huu na kusema kwamba inatakiwa watu tubadirike na kwenda na wakati hasa kutumia Fursa za mitandao ya kijamii. Mwingine alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro ambaye pia alijionea na kupata Maelezo Jinsi mtandao wa Mbeya yetu unavyo fanya kazi pia alitoa Pongezi zake kwa kazi kubwa inayofanywa na kutoa habari zenye uhakika zaidi.
Mgeni Rasmi wakati wa Kilele cha Nane nane mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Rajab Mwambungu amesema wamiliki wa mitandao ya kijamii nchini wanatakiwa kutumia nafasi waliyonayo kutangaza utanzania na uzalendo wao ndani na nje ya Nchi, Pia aliomba waandishi waige mfano wa Mbeya yetu Blog.
Wageni wengine waliotembelea katika Banda la Mbeya yetu ni Mkurugenzi wa Jiji Mbeya Mh. Mussa Zungiza , na Rais wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa Habari Nchini (UTPC) Kenny Simbaya.
Aidha kufuatia mchango huo wa Taso na wakulima kwa ujumla Uongozi wa Tone Multimedia Group Kupitia Mbeya Yetu Blog unatoa shukrani kwa wote waliuofanikisha shughuli za Nanenane hadi zinafikia kilele Agosti 8, na kupelekea kupata cheti cha ushindi.
Tunapenda kuwashukuru TASO kwa namna ya pekee , SBC (T) Ltd kupitia kinywaji chao cha Pepsi na wengine wengi ambao hatutaweza kuwataja majina lakini tunaahidi kuendelea kushirikiana kwa pamoja.
Pia tunapenda kuwashukuru Bloggers wote na waandishi wa habari kwa ujumla hatutaweza kutaja kila chombo lakini tumekuwa pamoja mpaka kufanikisha yote haya.
Mwisho kabisa Tunapenda kukushukuru wewe Mdau wetu Mkubwa wa Mbeya yetu Blog kwa kuonesha Moyo na Kutembelea kila wakati mtandao huu, Tunasema asanteni sana, Bila nyie sisi hatuwezi fanya kazi.
KWA PAMOJA TUUPENDE MKOA WETU WA MBEYA, KUPITIA MTANDAO WA MBEYA YETU BLOG.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni