Zahara Michuzi alipowasili katika ofisi za CCM mkoa wa Tabora ili kuchukua form ya kugombea viti maalum kwa vijana.
Zahara
Michuzi ni binti wa Issa Michuzi blogger na mpiga picha hodari wa rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye
anamalizia muda wake sasa.
Binti
wa Michuzi mara baada ya kuhitimu elimu yake ya shahada yake ya uchumi
UDOM ameona ni vyema akawatumikua wananchi wa nyumbani kwake mkoani
Tabora kwa kutangaza nia ya kugombea ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya
Chama Cha Mapinduzi.
Zahara Michuzi (kushoto) na Mwasham Hashim (kulia) karani wa UVCCM Tabora akitoa maelekezo ya uchukuaji wa form hizo.
Binti huyo wa Michuzi akikabidhiwa form yake leo katika ofisi za UVCCM mkoa-Tabora
Zahara akiifurahia form yake ya Ubunge wa viti maalum Tabora.
Zahara (kushoto) akilipia fedha halali ya form hiyo huku mama yake mlezi (katikati) akishuhudia kitendo hicho.
Zahara
sasa safari yake ya kuufukuzia ubunge wa viti maalu ndipo ikaanza huku
akiipitia form yake kwa mara ya kwanza toka azaliwe
Mwasham (kushoto) akitoa baadhi ya ufafanuzi kwa baadhi ya vipengele vilivyomo katika form hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni