Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya
Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa Panju akiongea na vyombo
mbalimbali vya habari ofisini kwake ,akitangaza rasmi kuwania kiti cha
ubunge jimbo la Arusha mjini kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM
kushoto ni mke wake.
Kassim Mamboleo ambaye ni katibu wa kamati ya ushindi ya mgombea Mustafa Panju akitoa utambulisho kwa vyombo vya habari.
Taswira katika mkutano huo na waandishi wa habari.
………………………………..
JIMBO la Arusha ni moja ya jimbo ambalo linaonekana kuwa ni jimbo
lenye siasa komavu, kutokana na hali hiyo limeonekana kuongoza kwa
vurugu na uvunjifu wa amani , ambapo kupitia kwa Mtangaza nia wa
ubunge jimbo la Arusha mjini Mustafa Panju amewahakikishia wananchi
kurudisha amani hiyo.
Jimbo hilo ambalo linashikiliwa na Mbunge wa Arusha mjini kupitia
chadema ,Godbless Lema ambaye hivi sasa ametangaza tena kulitaka jimbo
, ambapo hadi hivi sasa jumla ya wagombea 18 kupitia chama cha
mapinduzi wamejitokeza kumg’oa mbunge huyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati akitangaza nia ya
kuwania ubunge kupitia chama cha mapinduzi , Panju alisema kuwa ipo
sababu ya kurudisha jimbo hilo mikononi mwa CCM kwa kuwa CCM ni chama
kinachopenda amani na kinachodumisha amani.
‘kila mmoja anatambua jinsi ambavyo jiji la Arusha hivi sasa halina
amani kabisa na hakuna mtu anayedhubutu hata kutembea usiku , ila
nitahakikisha linakuwa jiji la amani na utulivu na kuwawezesha
wananchi wake kufanya shughuli zao bila hofu yoyote’alisema Panju.
Alifafanua zaidi kuwa,mbali na kurejesha amani jijini Arusha
atahakikisha anaondoa makundi mbalimbali yaliyopo miongoni mwa
wananchi kwa kuwafanya wawe wamoja na wenye ushirikiano ili kuleta
mabadiliko katika jimbo la Arusha kwa ujumla.
Pia alisema kuwa,wagombea wote wa nafasi ya ubunge katika chama ni
wajibu wao kujenga Undugu,Upendo, na urafiki wakati wote ili kuepuka
kujenga makundi ndani ya chama kwa misingi mbalimbali ya ukabila,
udini na hata urangi.
Panju alisema kuwa, swala la kuwepo kwa makundi na vikundi katika
vyama na kwa wananchi linapaswa kuangaliwa kwa umakini kwani
likiendelea kuwepo linajenga uhasama ndani ya chama na pia uhasama
unaoleta ubaguzi ndani ya nchi kwa ujumla .

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni