Mgeni
 rasmi ambae pia ni rais wa Makampuni ya Convivium Africa Investment, 
Ndg Alfonso ippolito akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa platform
 mpya ya matangazo iliyozinduliwa hapo jana katika hoteli ya 
serena.Paisha ni platform ya matangazo ambayo inapatikana kupitia simu 
za mkononi yaani smartphone na kupitia tovuti ambapo watumiaji wa simu 
za smartphone wanaweza kuipakua kupitia google play and playstore bure 
kabisa.
Meneja
 bidhaa wa Paisha, Godfrey Fataki akizungumzia jinsi paisha inavyofanya 
kazi na faida zake wakati wa uzinduzi wa platform hiyo uliofanyika jana 
katika hoteli ya serena
 Mgeni rasmi akifungua pazia kuashiria kuwa Paisha imezinduliwa rasmi 
Mtangazaji
 wa Redio Clouds Ephraim Kibonde akiwa katika picha ya Pamoja na Balozi 
wa Paisha wakati wa uzinduzi wa platform mpya ya matangazo 
iliyozinduliwa jana katika ukumbi wa Marquee Serena Hotel.
 Mdau
 akiwa pembeni ya mfano wa simu ya Iphone ambayo inaonyesha application 
ya Paisha.Paisha inapatikana kupitia playstore na google store bure na 
endapo utakuwa na application hiyo utaweza kufahamu na kupata huduma 
zote zitolewazo nchini huku wateja takribani Milioni 1 wameshajiunga 
huku watumiaji wakipata urahisi wa huduma hizo
tukipata selfie
 Black ryhino akipata selfie na mabest zake wakati wa uzinduzi huo
 Ni mwendo wa selfie tu
 Wadau wakifuatilia uzinduzi wa application ya Paisha
Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Paisha ni
 platform ambayo inapatika katika simu za smartphone pamoja na tovuti 
platform hii ni kwaajili ya watoa huduma na wauzaji wa bidhaa ambao 
wanapenda kuwafikia wateja wao kirahisi,Paisha inapatikana kupitia 
google play na playstore huku watumiaji wa paisha wananufaika kufahamu 
sehemu ambapo wanaweza kupata huduma mbalimbali kama vile maduka na hata
 huduma nyingine sehemu ambapo watuamiaji hao sio wenyeji au wenyeji 
lakini hawafahamu baadhi ya bidhaa zinapatikana wapi.
Ukiwa na 
application ya paisha katika simu inakusaidi kufahamu kuanzia ramani 
alipo mtoa huduma huyo pamoja na mawasiliano yake mfano umeenda tegeta 
na umepata pancha na haufahamu sehemu ilipo gereji ukiwa na paisha 
kwenye simu yako itakusaidia kufahamu ilipo gereji ambapo itakuonyesha 
jina la gereji iliyopo karibu na wewe hapo huku ikikuonyesha na ramani 
pamoja na mawasiliano ya gereji hiyo vilevile kwa bidhaa na huduma 
nyingine.
Ni 
application ambayo inawalete urahisi watumiaji na watangazaji wa bidhaa 
hizo kupitia paisha.kufahamu zaidi kuhusu paisha unachotakiwa kufanya ni
 tembelea tovuti yao yawww.paisha.co.tz na vilevile unaweza kupakua 
application hiyo kupitia playstore na google play sasa
Kuweza kupata faida zaidi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni