Mtaalam
kutoka Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC), Jumanne Shimba (kulia)
akielezea shughuli za kituo hicho kwenye banda la Wizara ya Nishati na
Madini.
Mtaalam
katika Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Rayson Nkya (kushoto)
akielezea sera ya madini kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara
hiyo kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mtaalam
kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Ayoub Shija akielezea
shughuli za mgodi huo katika banda la Wizara ya Nishati na Madini.
Mtaalam
kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Steven Lowoko akitoa maelezo
juu ya jinsi mtambo wa kufua umeme kwa kutumia maji unavyofanya kazi
kwa kutumia mfano wa mtambo huo kwa baadhi ya wanafunzi waliotembelea
banda la TANESCO.
Afisa
Mawasiliano kutoka Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia
ya Uziduaji Nchini (TEITI), Godwin Masabala akitoa maelezo jinsi
taarifa za mapato yatokanayo na rasilimali za gesi na madini
zinavyokusanywa.
Afisa
Huduma kwa Wateja katika Shirika la Umeme Nchini(TANESCO), Lucas Kusare
(katikati) akielezea shughuli za shirika hilo kwa mmoja wa wananchi
waliotembelea banda la Tanesco.
Afisa
Uokoaji katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Evarist Mwanakatwe
(kulia) akielezea shughuli za uokoaji zinavyofanyika katika mgodi huo
pindi majanga yanapojitokeza.
Baadhi ya wananchi wakiangalia aina mbalimbali za madini katika banda la Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST).
Mtalaam
kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Kankila Wakimbili akielezea
shughuli za wakala huo kwa wananchi waliotembelea banda hilo.
Mtaalam
katika Chuo cha Madini Dodoma(MRI), Mkunde Msaky (kulia) akielezea
fani zinazotolewa na chuo hicho kwa wananchi waliotembela banda hilo.
Wataalam katika Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) wakiwa katika picha ya pamoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni