Meneja Uhusiano wa Kampuni ya
Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi, akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa msimu mpya wa kandanda
kwa wateja wa DStv jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Masoko wa
Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kulia ni Meneja Mwendeshaji wa
Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.(Picha zote na Zainul
Mzige wa modewjiblog).
Meneja Uendeshaji wa Multichoice
Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo, akijibu maswali ya waandishi wa
habari (hawapo pichani) kuhusiana na huduma za DStv. Kushoto ni Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi.
Afisa Masoko wa Multichoice
Tanzania, Furaha Samalu, akielezea huduma za kuunganishwa kwa wateja
wapya wa DStv, ambapo ving'amuzi pamoja na dishi vinapatikana kwa
gharama nafuu kabisa ya Sh.99,000/- kwa mawakala wote wa DStv nchini.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya
Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi (wa pili kushoto) akikabidhi
zawadi ya begi kwa mwandishi wa habari, Joseph Michael baada ya
kuchezesha droo kwa waandishi waliohudhuria mkutano huo. Wanaoshuhudia
kushoto ni Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kulia
ni Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.
Furaha Samalu na Barbara Kambogi
wakikabidhi zawadi ya begi Super Sport kwa mpiga picha wa ITV, Abdallah
Kaniki aliyeibuka mshindi katika droo iliyochezeshwa na Multichoice
Tanzania wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Kulia Meneja
Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya
Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi akikabidhi zawadi ya T-shirts kwa
mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Imani Makongoro.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Andrew Chale, modewjiblog
Msimu mpya wa Soka 2015/16,
unatarajia kuanza rasmi Jumapili ijayo kwa kushuhudia ligi mbalimbali
Duniani zikichezwa na kurushwa moja kwa moja kupitia SuperSport
ambayo imejipanga kukuletea burudani kabambe kwa mashabiki wa soka
barani Afrika.
Meneja uendeshaji wa Multichoice
Tanzania , Ronald Baraka Shelukindo mapema jana akizungumza na vyombo
vya habari amebainisha kuwa, Wateja wa DStv wakae tayari msimu huu
kwenye Ulimwengu wa Mabingwa ambapo timu mbalimbali zimejiimalisha
katika kuakikisha zinatwaa ubingwa.
“Ligi ya mwaka zitakuwa za kasi na
kuvutia kwa kila timu. Barcelona wanajiandaa kutawala dunia kwa mara
nyingine, huku Manchester United wanahitaji kurudisha kiti chao cha
Ubingwa Uingereza. Jose Mourinho analenga kuhakikisha Chelsea inabaki
juu, wakati huo huo , Hispania inajiandaa kuhakikisha wanashinda kwa
mara ya tatu kombe la Euro 2016.” Ameeleza Baraka Shelukindo.
Ameogeza kuwa, Watazamaji wa
SuperSport watakuwa na nafasi ya kipekee kushuhudia mechi kwenye
ubora wa HD, ikiwa ni pamoja na michuano ya Ligi Kuu ya Uingereza
(EPL) , Ligi ya Hispania (La Liga) , Ligi ya Mabingwa wa Ulaya(UEFA) na
Ligi ndogo ya Ulaya ( Europa) ,mechi za FIFA za kirafiki za kimataifa
na Klabu Bingwa ya Dunia , Kombe la Ujerumani , Kombe la Mfalme
Hispania (Copa Del Rey) , Kombe la FA na zaidi.
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa
Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi anaeleza kuwa, Katika msimu huu ,
Ulimwengu wa Mabingwa itakuwa ikionyesha mechi zaidi ya 900 za
kimataifa. Wateja wa DStv Compact Plus wataweza kufurahia baadhi ya
mechi zaidi ya 450 ‘live’, huku Wateja wa DStv Premium watazawadiwa
mechi zote ‘Live’ zitakazorushwa katika chaneli zote za SuperSport .
“Kuanzia msimu huu na kuendelea,
vituko vyote vya Ligi Kuu ya Uingereza vitakuwa vikiletwa kwenu
kupitia SuperSport 5 ( SS5 ) inayopatikana kwenye kifurushi cha Premium.
SS5 sasa itakuwa ni nyumba ya soka la Afrika kwa ligi kuu ya Uingereza
huku ikijumuisha mechi 3 ‘Live’ kila Jumamosi na Jumapili.
Kuambatana na mechi kutakuwa na vipindi maalum vya soka kama PLTV
Kick Off, Match Day Live, Fan Zone, Saturday/Sunday Review, Football
Today, Classic Matches, Netbusters na Mech za Wiki” Amebainisha Barbara
Kambogi.
Moto wa La Liga utawashwa ndani ya
SuperSport 3 ( SS3 ). Chaneli hii itakuwa inakuletea mechi hadi tatu
za ligi ya Hispania ‘ Live’ kwa siku ya Jumamosi na Jumapili . Wateja
wa DStv Premium na Compact Plus watapata nafasi ya kuangalia mechi za
michuano ya Kombe la mashindano Uingereza ndani ya SS3 sambamba na
mechi za Jumamosi mchana za Ligi kuu ya Uingereza , mbadala wa mechi
inayorushwa ndani ya SS5, pamoja na Ratiba zote za Jumatatu usiku na
vipindi vya mahojiano vya studio.
Pamoja na Mechi za ‘Live’ ndani ya
SS3 , itakuwa inakuonyesha vipindi muhimu vya shoo za magazeti ,
yanayojiri ndani ya La Liga, pamoja na vipindi maalum vya ligi za soka
. Makombe yote ya mpira wa miguu, Mabingwa wa Ulaya na Ligi ya Europa,
Kombe la FA , Kombe la Mfalme Hispania (Copa Del Rey), Kombe la
Ujerumani , Euro 2016 na mechi za kirafiki za kimataifa zitaendelea
kutapatikana kwenye SS3 .
Kwa habari zaidi za michezo na ratiba za mechi kwenye SS5 na SS3, tafadhali tembelea www.supersport.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni