Mkurugenzi
wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la
Arusha kwa tiketi ya CCM akinadi sera zake mbele yawananchi na
wanachama wa chama hicho katika kata ya Moivaro ofisi za kata hiyo
jijini Arusha ili kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea wa ubunge
jimbo la Arusha kupitia CCM,aliwataka watanzania kuiga nyendo za Baba wa
Taifa Mwalimu Julias Nyerere kwa kuwa na upendo,ushirikiano na kukataa
rushwa(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM akicheza wimbo wa chama cha mapinduzi ,...CCM MBELE KWA MBELEEEEEEEEE ......kushoto kwake ni Mtia nia mwenzake wakili msomi Edimond Ngemela na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Monaban yajijini Arusha,Philemon Mollel ambaye pia ni Mgombea Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM
Mosses
Mwizarubi ambaye pia ni mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha
mapinduzi CCM akiomba ridhaa kwa wananchi pamoja na wananchama wa chama
hicho kuwatumikia katika nafasi ya Ubunge
Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju akimwaga
sera zake mbele yawananchi na wanachama wa chama hicho katika kata
Olorieni katika uwanja wa ccm,alisisitiza watu kujitolea kwa upendo kama
alivyofanya Baba wa Taifa hili Mwalimu Jualias Nyerere kwa kusimamia na kuweza kukomboa Nchi na hakukuwepo na swala la rushwa
Wakili msomi Edimond Ngemela anayeomba
ridhaa ya ccm katika nafasi ya ubunge akisalimiana na mmoja wa wananchi
waliojitokeza kuwasikiliza watia nia kupitia chama cha mapinduzi CCM
katika kata ya Olorieni jijini Arusha
Mohamed
Omary ambaye pia ni mgomea Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM
akimwaga sera zake ambapo alisema kuwa akipata ridhaa ya kuwatumikia
atahakikisha anawachukulia hatua kali wale wote wanaotelekeza watoto
hali inayosababisha watoto wa mtaani kuongezeka
Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi akiongea katika mkutano huo
Katibu
wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano ambaye pia ni msimamizi wa
uchaguzi kulia akiwa na mmoja wa wagombea mapindizi Mosses Mwizarubi
Mtia
nia ya Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM Thomas Munisi akimwaga
sera zake katika kata ya Moivaro akiomba ridhaa ya kwa wananchi ya
kuwatumikia katika nafasi ya ubunge jimbo la Arusha mjini
Taswira katika kata ya Moivaro jijini Arusha
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni