Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
imeadhimia kuhusisha Sekta binafsi pamoja na benki nchini ili kuongeza kasi ya usambazaji
umeme Vijijini.
Hatua hiyo itasaidia kuleta maendeleo
ya haraka na kufikisha umeme katika maeneo ya vijijini katika maeneo mengi hapa
nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini
Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava wakati akiongea katika
kikao kilichohusisha Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini, sekta binafsi pamoja
na benki zilizopo nchini.
Amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa
Wakala wa Nishati Vijijini , kasi ya upelekaji umeme vijijini hapa nchini imeogezeka.
“Baada ya hiki chombo kuingia
kazini kasi imeongezeka kwani kwa sasa wananchi waliofungiwa umeme ni zaidi ya
asilimia 24 na wakati ule namba ya uwepo wa umeme vijijini ilikuwa asilimia 10
mwaka 2005 ambapo kwa sasa ni karibu asilimia 40 na tunatarajia kuongeza kasi
hii kadri tunavyozidi kupata vyanzo vingi vya fedha kwani malengo yetu hapo
baadaye ni kuweza kufikia asilimia zaidi ya 70”, alisema Mhandisi Mwihava.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa
Nishati Vijijini, Dkt. Lutengano Mwakahesya ameeleza kuwa kikao hicho kinalenga
kufafanua namna gani sekta binafsi
zinavyoweza kupata faida kwa kuingia katika sekta ya nishati pamoja na
kushirikia katika kuleta maendeleo ya haraka katika kufikisha umeme kwa
asilimia 60 na zaidi.
Amesema kuwa endapo umeme nchini
utaenea katika maeneo ya vijijini utaweza kuleta maendeleo makubwa hususani
katika kuleta ajira kwa vijana na kuibua miradi mbalimbali kupitia viwanda
vidogo vidogo jambo ambalo litapunguza tabia ya baadhi ya watu kukimbilia
mijini katika kusaka ajira.
“Maendeleo makubwa yatapatikana
iwapo umeme huu utafika vijijini, utasaidia kuleta viwanda vido vidogo kama
vile mashine za kukoboa ili ipatikane ajira vijijini na watu waache kuhamia
mjini nkutafuta maisha bora kwanbi umeme huu utasaidia wawananchi kuibua miradi
mizuri ya maendeleo”. Alisema Mwakahesya.
Ameongeza kuwa, watu wengi
hawawezi kulipa shilingi 27,000 hivyo Bodi hiyo inatazamia kuongea na benki za
zilizopo nchini pamoja na sekta binafsi ili kuweza kupata njia bora zaidi za
kufikisha umeme katika maeneo hayo ya vijijini kwa kuwapa mkopo ambao unaweza
kulipwa pole pole kwa kutumia kulipia bili za umeme.
Serikali ilikamilisha mchakato wa
uanzishwaji wa Taasisi ya Wakala wa Nishati Vijijini mnamo mwaka 2005 ambapo
mwaka 2007 hadi hivi sasa baada ya Wakala kuingia kazini, kasi ya upelekaji ya
umeme vijijini imekuwa kubwa.
Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na Baadhi ya wadau wa Sekta binafsi pamoja na benki
zilizopo nchini wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere
jijini Dar es Salaam kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) juu ya kuleta
maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini .
Baadhi ya
wadau wa Sekta binafsi pamoja na benki zilizopo nchini wakifuatilia ajenda
wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaam kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) juu ya kuleta maendeleo ya
usambazaji wa umeme vijijini .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni