katika picha ni mwanadada
Phidesia Mwakilima
Phidesia Mwakilima
Mkurgenzi wa kampuni ya Phide Intataiment ambaye pia ni meneja masoko wa kituo cha redio Triple A ya Arusha, Phidesia Mwakilima, ameibuka kidedea kwenye uchaguzi wa mbunge viti maaluimu kupitia jumuia ya wazazi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha.
Phidesia Mwakilima, amepata kura 18 na kuwashinda, Aimbora Nnko, aliyepata kura 6, Angela Mwanri kura 4 na Anna John kura 2 ,uchaguzi huo umefanyika ukumbi wa ccm, mkoa.
Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo katibu wa jumuia ya wazazi mkoa, wa Arusha, Mayasa Kimbau, amewataka wale ambao kura zaohazikutosha kutokukata tamaa bali wajipange kwa chaguzi zingine ndani ya chama.
Akawataka wanawake wasiwe wanyonge kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi bali wawe mstari wa mbele kujitokeza kila uchaguzi utakapotokea
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni