Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea wakati wa
ufunguzi wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars kwa viongozi wa
mikoa iliyofanyika leo (Julai 7, 2015) jijini Dar es Salaam. Katikati
ni Mwenyekiti soka la vijana wa TFF Ayoub Nyenzi na Kushoto ni
Mwenyekiti msaidizi soka la vijana wa TFF Khalid Abdallah.
Mkurugenzi wa ufundi wa TFF Salim Madadi akiongea wakati wa wa semina
elekezi ya Airtel Rising Stars kwa viongozi wa mikoa iliyofanyika leo
(Julai 7, 2015) jijini Dar es Salaam. Katikati
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akifatiwa na
Mwenyekiti soka la vijana wa TFF Ayoub Nyenzi.
Viongozi soka kutoka katika mikoa inayoshiriki michuano ya Airtel
wakifatilia Seminar elekezi ya Michuano ya Airtel Rising Stars
iliyofanyika iliyofanyika leo (Julai 7, 2015) jijini Dar es Salaam.
Mikoa inayoshiriki katika michuano ya mwaka huu ni pamoja na ya
Mwanza, Morogoro, Mbeya, Temeke, Ilala and Morogoro kwa upande wa
wasichana huku mikoa ya Ilala, Kinondoni, Temeke, Mbeya, Mwanza and
Arusha ikiwa ni kwa upande wa wasichana.
Mwenyekiti soka la vijana wa TFF Ayoub Nyenzi akitoa ufafanuzi wa
jambo wakati wa Semina elekezi ya michuano ya Airtel Rising Stars
iliyoshirikisha wasimamizi na viongozi wa mikoa itakayoshiriki katika
michuano ya Airtel Rsing Stars inayotegemea kutimua vumbi 20 Julai.
Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando na kulia
ni baadhi ya viongozi wa TFF.
Shirikisho la Soka nchini (TFF), limewasisitiza viongozi wa soka ngazi
za mikoa kutambua kuwa lengo kuu la michuano ya Airtel Rising chini ya
vijana wa miaka 17, ni kuibua vijana kwa manufaa ya Taifa kwa baadaye
na sio kulelekeza nguvu zao katika kupata matokeo mazuri uwanjani kama
ambavyo watu wengi hufikiri.
“Tumegundua kwamba baadhi ya viongozi wa soka mikoani wana fikra
tofauti na lengo la michuano hii, wao huangalia zaidi kupata matokeo
mazuri uwanjani kuliko kutafuta vijana wenye vipaji kama lilivyo lengo
la michuano hii. Na hii ndio sababu kuu ya ongezeko la tatizo la watu
kuleta vijana waliozidi umri uliolengwa katika program hii”, amesema.
Mwesigwa amemimina pongezi kwa kampuni ya Airtel nchini kwa kuamua
kuwekeza katika soka hapa nchini hasa la vijana. “ Michuano ya Airtel
Rising Stars imekuwa ni chachu kubwa hasa kwa upande wa soka la
wanawake, ambapo idadi kubwa ya wachezaji wanatokana na progamu hii”,
amesema Mwesigwa.
Ameongeza kuwa soka la vijana limekuwa ni njia ya uhakika na endelevu
katika maendeleo ya soka hapa nchini. “Kwa mfano nchi ya Cameroon,
wamepata mafanikio makubwa na ya kuvutia kutokana na kuwekeza katika
program za vijana”, alisema, huku akiiongeza pia Hisapania kama nchini
nyingine ambayo ilifanya hivyo na kufanikiwa kuchukua kombe la dunia.
Mwesigwa amewataka viongozi wa soka ngazi mbalimbali nchini kufuata
taratibu na kanuni za michuano hii. “Nataka muelewe kuwa hii ni
program muhimu na nyeti sana kwa taifa, kwa sababu inalenga hasa
vijana ambao wanahitaji uangalizi wa karibu sana ili kutimiza ndoto
zao.
Kama ukiwafundisha kuwatii waamuzi, basi watafanya hivyo katika
kipindi chote cha maisha yao ya soka, na endapo ukiwafundisha
kutowatii waamuzi basi pia watafanya vivyo hivyo,”alisema huku
akiwaonya vikali viongozi kutowapandikiza wachezaji imani za
kishirikina.
Michuano hiyo imepanga kuanza kutimua vumbi katika ngazi ya awali
(mikoa) julai 20 na kuhitimishwa Agusti 30, ambapo ngazi ya taifa
itaanza Septemba 11 hadi 21 jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Meneja Mahusiano wa Aitel nchini Jackson Mmbando
amesema kuwa hii ni fursa nyingine tena adhimu kwa vijana kuonesha
vipaji vyao ambavyo vitawawezesha kutimiza malengo yao ya baadaye
kupitia mchezo wa soka.
Airtel Rising Stars mwaka huu inaenda bega kwa bega na kampeni mpya
inayojulikana kwa jina la ‘It’s Now’ huku nahodha wa Ivory Coast
ambaye pia ni kiungo wa Manchester City Yaya Toure akiongoza kampeni
hiyo. Kampeni hii inalenga kulea na kukuza vipaji barani Afrika
kupitia nyanja mbalimbali kama vile michezo, mtindo wa maisha na
mziki lakini vilevile kuwapa mbinu zitazaowawezesha kupata ufumbuzi wa
masuala ya kiteknolojia na kuona fursa zinazowazunguka.
Michuano ya Airtel Rising Stars mwaka huu itajumuisha mikoa ya Mwanza,
Morogoro, Mbeya, Temeke, Ilala and Morogoro kwa upande wa wasichana
huku mikoa ya Ilala, Kinondoni, Temeke, Mbeya, Mwanza and Arusha ikiwa
ni kwa upande wa wasichana
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni