Mkuu
 wa kituo cha Kulelea Watoto yatima cha Al-Madina, Bi. Kulthum Juma 
akizungumzia kuhusu kituo hicho pamoja na kutoa shukrani kwa kampuni ya 
Multichoice Tanzania kwa kuendelea kukisaidia kituo cha hicho ambacho 
kina takribani watoto 68 na pia kituo hicho kipo eneo la Tandale kwa 
Tumbo jijini Dar.
Ustadhi Mashaka Salim akitoa neno.
Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania, Peter Fauel akichukua chakula wakati wa kuwafuturisha  watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Al-Madina kilichopo Tandale kwa Tumbo, Wa pili kutoka kulia ni Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo.
Meneja
 Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi, akitoa 
huduma ya chakula kwa watoto yatima hii ikiwa ni njia mojawapo ya 
kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Baadhi
 ya Watoto yatima, Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania pamoja na 
viongozi wa kituo hicho cha Al-Madina wakichukua chakula katika futari 
iliyoandaliwa na kampuni ya Multichoice Tanzania.
Baadhi
 ya Watoto yatima, Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania pamoja na 
viongozi wa kituo hicho cha Al-Madina wakijumuika katika futari hii 
ikiwa ni moja wapo ya kutoa msaada katika vituo mbalimbali hapa nchini.
Meneja
 wa Fedha wa Multichoice Tanzania, Francis Senguji akitoa neno la 
shukrani kwa niaba ya Kampuni ya Multichoice Tanzania kwa waliofika na 
kujumuika nao katika futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice 
Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni