Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
akilifungua rasmi Jengo Jipya la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
Tanzania { COSTECH} Ofisi ya Zanzibar
liliopo ndani ya majengo ya zamani ya ilichokuwa kiwanda cha Sigara Maruhubi
Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif wa pili kutoka Kushoto akipata maelezo kutoka kwa
Wataalamu wa Chuo cha Utafiti Kizimbani wakiongozwa na Said Suleiman
Bakari jinsi zao
la viazi vitamu linavyoweza kutumiwa vyema katika utengenezaji wa Juisi. Wa kwanza
kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Majini Magharibi Mh. Abullah Mwinyi.
Watafiti na wawakilishi wa Vikundi vya wajasiri amali waliopata ufadhili
kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia wakimpatia maelezo Balozi Seif
wakati akiangalia maonyesha mara baada ya kulifungua Jengo la Tume hiyo.
Baadhi ya Wataalamu na wajasiri amali kutoka vikundi tofauti Nchini
wakifuatilia matukio mbali mbali yaliyojiri kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo
Jipya la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia { COSTECH }.
Balozi Seif akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Jengo la Tume ya Taifa
ya Sayansi na Teknolojia hpo Maruhubi akimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la MapinduziI Dr. Ali Mohammed Shein.
Balozi Seif akiwa katika Picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Tume ya
Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania { COSTECH } mara baada ya uzinduzi wa
jengo la Tume hiyo hapo Maruhubi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein alisema wakati umefika kwa sekta binafsi
kujenga Utamaduni wa kutoa ruzuku za tafiti kwa Tume ya Taifa ya Sayansi na
Teknolojia ili ijipatie nguvu za ziada za uwezeshaji wa kuendesha shughuli zake
za utafiti kama nchi nyengine Duniani zilizofanikiwa kwa kufuata mfumo huo.
Alisema kufanya utafiti kunahitaji nguvu kubwa ya
fedha kiasi kwamba Serikali pekee haiwezi kumudu kugharamia bila ya
kushirikisha taasisi mbali mbali za sekta binafsi za ndani na nje ya nchi.
Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein alisema hayo
katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi wakati wa ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Tume ya Taifa ya
Sayansi na Teknolojia { COSTECH } liliopo Maruhubi nje kidogo ya Mji wa
Zanzibar.
Alisema Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
Tanzania imeonyesha mwanga wa kusaidia jamii kwenye tafiti za kina za
Kimaendeleo zitakazomkomboa Mtanzania kutoka katika dimbwi la umaskini na
kuelekea kwenye maendeleo ya kweli.
Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi
na Teknolojia COSTECH Dr. Hassan Mshimba
alisema ujenzi wa Ofisi ya Tume hiyo hapa Zanzibar ni kutekekeza ahadi iliyotoa Uongozi wa
Taasisi hiyo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mwaka 2012.
Mkurugenzi Mkuu huyo wa Costech alisisitiza kwamba katika
azma ya kukuza ajira Nchini Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia imekusudia
kuungana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha vitengo vya
Utafiti Zanzibar kama alivyosisitiza Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein
siku ya Utafiti Tarehe 12 Disemba mwaka 2014.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Sayansi
na Teknolojia Kanal Mstaafu Joseph Simba Kalia ameipongeza Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar kwa ukarimu wake wa kutoa
Jengo kwa ajili ya Ofisi za Tume hiyo.
Kanal Mstaafu Simba Kalia alisema kitendo hicho
kilichofanywa na SMZ ni uthibitisho wa
kuthamini umuhimu wa fani ya Utafiti ambayo ndio chachu ya maendeleo ya jambo
lolote lile hapa Ulimwenguni.
Ofisi ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojiaawali
ilizinduliwa rasmi mnamo Tarehe 11 Juni Mwaka 2012 katika
Majengo ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania yaliyopo Tunguu Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar na kuanza kutoa huduma
zake hapa Zanzibar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni