Usili
wa kwanza wa Dance 100% (2015) umefanyika kwa mafanikio makubwa Temeke
jijini Dar es Salaam, ambapo makundi ya Team ya Shamba, The WT Group,
WD, The Best Boys Kaka Zao na Team Makorokocho wameweza kushinda nafasi
ya kuingia katika michuano kutoka wilaya ya Temeke.
Makundi
haya yamechuana vikali na mengine 6 yanayokamilisha idadi ya makundi
11, UNI 6 Crew, GMF Crew, TWC, Dar Crew, Noma Sana Crew, na Viga Stars
yaliyojitokeza kuwania nafasi hiyo katika usajili huo wa kwanza.
Mratibu
wa mashindano hayo kutoka East Africa Television na East Africa Radio,
Bi Happy Shame, amesema kuwa amefurahishwa na utulivu na amani ambayo
wapenda burudani Temeke wameonyesha leo, huku pia kukiwa na vipaji
mbalimbali kutoka makundi yaliyojitokeza katika usaili huo wa kwanza.
Akizungumza
baada ya kumalizika michuano ya usaili huo, mratibu wa Dance 100%
kutoka BASATA, Kwerugira Maregesi, mbali na kufurahishwa na vipaji
vilivyojitokeza, amekumbushia umuhimu wa makundi hususan yale
yanayotarajiwa kushiriki usajili unaofuata, kuzingatia vigezo na
masharti yaliyowekwa kujiwezesha kushinda, ikiwepo ubunifu katika
mitindo ya kudansi, kuburudisha na muonekano, huku akishauri kupunguzwa
kwa mitindo ya sarakasi na kuongezwa ladha katika upande wa dansi zaidi.
Majaji
Super Nyamwela, Queen Darleen na Shetta wametumia umakini nkubwa
kuhakikisha wanatoa alama zinazostahili kwa mujibu wa vigezo kwa
washiriki wote, huku burudani mbalimbali zikijiri zikishereheshwa
kikamilifu na watangazaji rasmi wa Dance 100 kwa mwaka huu, T-Bway 360
na mrembo Maggie Vampire.
Majaji
pia kila mmoja kwa nafasi yake wametaka washiriki watakaoendelea
kujitokeza kujipanga zaidi wakizingatia vigezo vilivyowekwa, ambavyo
ndivyo wanavyovitumia kutoa maksi (alama) zitakazowawezesha kufikia
ushindi.
Usajili
wa pili wa mashindano haya makubwa kabisa ya kudansi utafanyika katika
viwanja vya Don Bosco Upanga siku ya Jumamosi Tarehe 01 Agosti 2015,
ambapo makundi mengine matano yatasakwa kushiriki katika michuano hiyo
kwa mwaka huu.
Usikose
kujionea kwa urefu yote yaliyojiri pale TCC Chang'ombe katika
mashindano ya usajili huo, kwa kutazama ting'a namba moja kwa vijana
EATV, siku ya Jumamosi, kuanzia saa 12 na nusu jioni.
East
Africa Television na East Africa Radio inaleta Dance 100% kwa kupewa
nguvu na mtandao wa Vodacom Tanzania na Coca Cola ambao ndio kinywaji
rasmi cha dance 100% (2015).
PICHANI
JUU: Kati ya makundi matano yaliyopita kwenye usaili wa kwanza wa Dance
100% (2015) - Temeke. Kundi linaitwa 'The Best Boys Kaka Zao'
Kutoka
kushoto -Majaji wa mwaka huu kwenye Dance 100% ni Super Nyamwela,
Shetta na Queen Darleen wakiwa wanajumulisha matokeo ya washiriki kutoka
Temeke.
Shabiki
wa kundi la 'Noma Sana' akiwa anajitayarisha kushangilia timu yake
kwenye usaili wa kwanza Temeke kwenye Dance 100% (2015)
Washiriki wa kundi la 'Noma Sana' mwaka huu kwenye Dance 100% wakiwa wanafanya yao viwanja vya TCC Changombe.
Watangazaji
rasmi wa Dance 100%, TBway 360 na Maggie Vampire wakiwa wanasherehesha
kikamilifu huku burudani mbalimbali zikijiri TCC Changombe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni