Japo kumekuwa na stori nyingi zinazohusu
 ajali za ndege, bado sifa ya kuwa usafiri salama namba moja duniani 
haijaharibika, nimezipata hizi pichaz na video zinazoonesha Rubani 
ambaye alijiongeza na kuona bora aishushe ndege katikati ya barabara ya 
magari iliyopo Stafford, New Jersey Marekani.
Polisi wa Stafford waliweka Video mtandaoni ikionesha tukio lote lilivyotokea, ndege ilikuwa imebeba Wanafunzi wa Skydive East Coast ambao hawakutajwa walikuwa ni wangapi, ila alikuwepo Mwalimu wao mmoja ambaye alipata jeraha mkononi.. hakuna mtu mwingine aliyejeruhiwa kwenye tukio hilo.
Chanzo cha ajali kinachunguzwa ila kwa ripoti iliyotoka mpaka sasa hivi ni kwamba ndege ilipata hitilafu kwenye Engine ikabidi ishushwe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni