KABLA YA KAMATI KUU CCM KUPIGA PANGA MAJINA YA WAGOMBEA, UVCCM NYAMAGANA WAMWAGA UGALI WA LOWASSA. Wednesday, July 08, 2015 No comments Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Hussein. A. Kimu amemshutumu waziwazi bila kigugumizi mtangaza nia Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kwa kumhusisha na mipango ya kuaandaa kundi la Mabaunsa na Machinga wa mkoa wa Mwanza kwa lengo la kwenda mjini Dodoma, kushinikiza viongozi wa chama hicho kumchagua mgombea wao na kundi jingine la vijana na akina mama wa CCM kusimama njiani kusimamisha misafara ya wajumbe wa NEC, na Mkutano mkuu wa Chama Taifa kuwapa shinikizo na vitisho wakiwalazimisha warudi na jina la mgombea wao ndugu Edward Lowassa. Mwenyekiti huyo wa vijana wilaya ya Mwanza mjini (Nyamagana) ameongeza na kudai kuwa yote hayo yalipagwa kufanyika kwa malipo, na kila kijana aliwekewa ahadi ya kulipwa Tsh 100,000/= kwa kila siku, kwa siku zote mpaka mpango ukamilike ... BOFYA PLAY KUSIKILIZA Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Hussein. A. Kimu. YAH.TAMKO LA KUPONGEZA KAULI YA MKUU WA MKOA WA MWANZA NDUGU STANSLAUS MAGESA MULONGO. Ndugu wanahabari na watanzania wote. Kwanza nitumie fursa hii kuwashukuru kwa kuitikia wito na kukubari kuja kuungana nasi kwa lengo la kuwajuza watanzania kwa kile kinachoendelea katika mkoa wetu Wa mwanza kwa faida na manufaa ya watanzania wote. Siku ya 6/7/2015, mkuu wetu wa mkoa Wa mwanza alitoa maelekezo kwa makamanda wa polisi kuzuia watu wasio kua na malengo mazuri kwa nchi yetu na taifa letu. Wanao kwenda Dodoma kwa lengo la uvunjifu wa amani,katika kipindi hiki cha mchakato wa vikao vinavyoendelea vya kuchuja na kupata kiongozi atakae peperusha bendera ya chama cha mapinduzi, Huo ni wajibu wake akiwa ni mwenyekiti Wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa, na ndio muwakirishi Wa rais kwa ngazi ya mkoa anawajibu na kila sababu ya kukemea, kuonya, kushauri na kuelekeza mambo yote yanayohusu raia na Mali zao hivyo sisi wana mwanza na watanzania kwa ujumla hatukuona ubaya wa aina yeyote kwa kauli ya mkuu wetu wa mkoa. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Hussein. A. Kimu (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Wamachinga mkoa wa Mwanza Iddi Tembo (kulia) na mkuu wa kundi lisilo rasmi la mabaunsa mkoani Mwanza, Mbayi Kambarage (kushoto) Wanahabari kikazi zaidi. Cha kusikitisha Jana 7/7/2015. Kuona katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari mtu anae jiita mtemi Sylvester Yared, ambae ndiye mratibu Wa genge la vijana wahuni wanaojiita 4U movement. Akidhihaki na kupinga tamko la mkuu wetu Wa mkoa wa Mwanza. Binafsi nilishitushwa sana..... Katika Katiba yetu ya chama cha mapinduzi na kanuni zake tuna jumuiya tatu 1.Jumuiya ya wanawake(UWT) 2.Jumuiya ya wazazi 3.Jumuiya ya vijana (UVCCM) Ndani ya chama cha mapinduzi hatuna taasisi wala jumuiya inayoitwa 4Umovement. Swali la kujiuliza jeuri, kiburi na mamlaka ya kuunda chombo kisicho rasmi chenye lengo la kuvuruga,kuhatarisha mustakabari wa chama chetu na Taifa letu kwa maslahi ya mtu binafsi,anaetumia kundi la vijana wasio jitambua kwa gharama yeyote ili aingie ikulu,na huyu si mwingime bali ni ndugu Edward Lowasa. Ninayaongea haya kwa ushahidi, ninao hapa viongozi wawili kutoka kundi la mabaunsa na machinga, wa mkoa wa mwanza ambao walifatwa na kupewa kazi ya kuandaa na kukusanya vijana wasiojielewa kwa lengo la kwenda Dodoma. Kushinikiza viongozi Wa chama kumchagua mgombea wao, na kundi jingine la vijana na akina mama Wa CCM kusimama njiani kusimamisha misafara ya wajumbe Wa NEC, na mkutano mkuu wa chama Taifa kuwapa shinikizo na vitisho, kwamba lazima warudi na mgombea wao ndugu Edward Lowassa. Wanahabari kikazi zaidi. Hayo yote yanafanywa kwa malipo, Na kila kijana atalipwa tsh 100,000.kwa kila siku ,kwa siku zote atakazo fanya kazi, mpaka kieleweke. Ndugu wanahabari Mimi kijana mzalendo wa Tanzania ninapata wakati mgumu na Mashaka makubwa pindi ninapo ona mtu ambae hakubaliki katika jamii ya watanzania mwenye madoa na kashfa chungu nzima tena afya yake ikiwa ya kususua analazimisha kwa kutumia gharama kubwa ili afike Ikulu mtu huyu kwa kauli ya hayati baba Wa Taifa,namnukuu, Tumuogope kama ukoma hafai.mwisho wa kunukuu. Nimalizie kwa kuwashukuru na kuwapongeza viongozi wetu wakuu wa chama na serikali kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kujenga na kuimarisha chama na serikali kwa kutatua na kusimamia maslah ya watanzania, Mwisho kwa nafasi ya kipekee niwashukuru wanahabari wote mlio hudhuria na watanzania wote mnao nisikiliza na kunitazama.Mungu kibariki chama chetu CCM, Mungu ibariki Tanzania. Imeandaliwa na Hussein. A. Kimu Mw/kiti UVCCM(W) Nyamagana Mwanza. Albert G.Sengo SABASABA WINDHOEK LUNCH PARTY ILIVYOJUMUISHA WADAU WA VIP WAKITAIFA NA KIMATAIFA KATIKA UKUMBI WA DANKEN HOUSE MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM Wednesday, July 08, 2015 BIASHARA No comments Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited James Rugemalira akitangaza nia na kuwakaribisha wageni mbalimbali katika hafla hiyo ya Sabasaba Windhoek Lunch Party. Bwana Rugemalira (kulia) akimweleza jambo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kansa kutoka nchini India Profesa. Antony Pais walipokutana katika hafla hiyo. Bwana James Rugemalira (kulia), akiteta jambo na Mwenyekiti wa Ukanda Maalumu wa Kiuchumi Mkoa wa Tanga, Chris Incheul Chae ambaye pia hakukosa kuhudhuria hafla hiyo. Bwana Rugemalira (kulia ) akisalimiana na Mwanyekiti wa Kamati ya Mahusiano na Umma wa Kampuni ya Mabibo Beer wines and Spirits Limited, Anic Kashasha. Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Secelela Balisidya naye alikuwepo kuhakikisha mambo yanaenda sawa. Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Alice Marco (kulia) naye alikuwepo kuhakikisha kila mgeni anapata vinywaji vya Windhoek vya kutosha. Hakuwa na mzaha katika swala hilo. Mdau Faustine Kapama (kushoto) na mawakili Paschal Kamala na Sosten Mbedule walikuwepo kufurahia kinywaji murua cha Windhoek. Ni wageni wengi walikuwepo kuhudhuria hafla hiyo. Unaona mambo yanavyochangamsha? ni Windhoek tu kwa kwenda mbele. Huwezi kuamini ilikuwa furaha kila kona. Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Benedicta Rugemalira (kushoto) na mwanasheria wa kampuni hiyo, Respicius Didace (kulia) wakiwa na wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi walipohudhuria hafla hiyo. Dk. Dee (kulia), akiwa na madaktari wengine katika hafla hiyo. Albert G.Sengo ZOEZI LA UBORESHWAJI DAFTARI LA WAPIGAKURA LAENDELEA MKOANI PWANI, RAIS JAKAYA KIKWETE AJIANDIKISHA KUPITIA BVR KIJIJINI MSOGA


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa kielektoniki(Biometric Voters Register( BVR) katika kijiji cha Msoga,kata ya Msoga wilayani Bagamoyo leo.Kulia akiangalia kwa makini ni mwandikishaji msaidizi Bi.Happyness Thomas Misana na katikati ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi Tume ya Taifa Uchaguzi Bi.Mariam Rajabu.Kushoto aliyesimama akishuhudia ni Mbunge wa Chalinze Ridhwani Kikwete.
 Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Uchaguzi Taifa ya Uchaguzi Bwana Sanif Khalfan akichukua lama za vidole vya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kijijini kwake Msoga wilaya ya Bagamoyo leo .
 Bwana SANIF Khalfan ambaye ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi akimpiga picha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kupiga kura kwa kutkumia teknolojia mpya ya BVR kijijini Kwake Msoga leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitambulisho chake wakati wa zoezi la kujiandikisha kijijni kwake Msoga leo.
 Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya Rais Kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo.
Rais Kikwete akimshukuru Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva baada ya kukabidhiwa kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo. Picha na Freddy Maro.
Rais akuonyesha kitambulisho chake alichopewa mara baada ya kujiandikisha katika daftari daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo.
---
JUMLA ya watu milioni 11,248,194 wameandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura zoezi ambalo linaendelea kwa sasa hapa nchini likiwa limeingia mkoani Pwani.

Hayo yalisemwa leo kwenye Kijiji cha Msoga kata ya Msoga wilayani Bagamoyo na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Damian Lubuva alipokuwa anampa taarifa Rais Dk Jakaya Kikwete mara baada ya kujiandikisha.

Bw. Lubuva alisema kuwa malengo ni kuandikisha watu milioni 21 hadi 23 kote nchini mara zoezi hilo litakapokamilika kati ya Julai mwishoni au Agosti mwanzoni kama hakutatokea matatizo.

“Hadi sasa ni mikoa 11 inaendelea na zoezi ambayo ni Mwanza Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro Morogoro na jana ulianza mkoa wa Pwani,” alisema Lubuva.

Aidha alisema kuwa changamoto zilizojitokeza ni za kawaida hasa kutokana na mfumo huu kuwa ni mpya kwani kila jambo jipya lina changamoto zake.

“Mfumo huu ni mpya hivyo lazima kuwe na changamoto za hapa na pale lakini zoezi linakwenda vizuri na tunaamini kuwa tutafanikiwa kama tulivyopanga,” alisema Lubuva.

Mkoa wa Pwani una jumla ya vituo 1,752 na mashine za BVR 932 ambapo kata ya Msoga kuna jumla ya vituo 17 zoezi hilo kwa mkoa wa Pwani lilianza jana na litamalizika Julai 20.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni