Mtoa
mada Awadh Ali Said, akitoa mada kuhusu muungano na umuhimu wa
kuzingatia misingi ya amani katika mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi
ya Mwalimu Nyerere ambao ulifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius
Nyerere Dar es Salaam leo.
Mtoa
mada Dk. Humphrey Polepole akitoa mada kuhusu kuzingatia misingi ya
amani na umoja wa taifa letu kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akitoa majumuisho
ya jumla juu ya dhima ya mdahalo huo, ambapo aliwataka watanzania
kuendelea kupiga vita rushwa na kusisitiza kutowachagua watoa rushwa
katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku (kushoto),
akiteta jambo na watoa mada katika kongamano hilo, Jaji mstaafu Joseph
Warioba na Dk.Humphrey Polepole (katikati)
Jaji mstaafu Joseph Warioba, akimuonesha Dk. Humphrey Polepole ujumbe mfupi aliotumiwa kwenye simu yake .
Jaji mstaafu Joseph Warioba akisalimiana na washiriki wa mdahalo huo baada ya kumalizika. Mdahalo huo uliorushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV. |
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Jaji mstaafu Joseph Warioba (kulia), akiwaaga washiriki wa mdahalo huo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni