Fanisi kutumia dola 6m kusaidia wasindikaji wa Tanzania


fanisi
Muasisi na mwenyekiti wa Kijenge, Andrew Mollel.
*Fanisi Venture Capital Fund imetoa dola za Kimarekani milioni 6 kwa maendeleo ya kampuni ya  Kijenge Animal Product Limited.
Kijenge ni kampuni mseto ya usindikaji iliyopo mkoani Arusha,ambayo inajihuhisha na usagaji mahindi, uzalishaji wa chakula cha wanyama na kuku ambao wako tayari kwa kula, kilimo na usindikaji. Kampuni hiyo iko katika mchakato wa kujenga msingi kwa ajili ya awamu nyingine ya ukuaji ambapo kutakuwa na ongezeko la vyanzo mbalimbali vya  mapato yake kwa kuboresha miundombinu yake ya sasa ya uzalishaji ikiwa ni pamoja na kuanzisha njia mpya za uzalishaji.Fanisi itakuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha inasaidia ukuaji wa kampuni katika hatua ijayo na pia kutoa fedha za mtaji kwa ajili kukuza hisa za Kijenge.
Akizungumzia juu ya zoezi hilo, Muasisi na mwenyekiti wa Kijenge, Andrew Mollel amesema: “Baada ya mazungumzo binafsi ya miaka kadhaa ya kuhakikisha hakuna anayepunjwa, tumeona kuwa Fanisi ni watu sahihi kwa maendeleo ya Kijenge, na mtazamo wao ni zaidi ya msaada wa kifedha wanaotoa. Ubia huu unatupa fursa ya kukuza mtaji wetu ambao utatusaidia kuboresha mbinu za usambazi bidhaa zetu ili kukidhi mahitaji ya wateja kwa usahihi”.
Mkurugenzi mwenza wa Fanisi Tony Wainanina amefurahiswa na mkataba huo pamoja na ari kubwa ya kijasiriamali ambayo kampuni imefaidika ikiwa chini ya uongozi wa Mollel. Wainanina amesema: “Tunaiunga mkono kampuni yenye historia na jina kubwa katika soka la hapa nchini. Huu ndio mkataba wa kwanza ambao tumefanikiwa kufikia makubaliano ambao tutakua tukiangazia katika masula ya kilimo cha biashara hasa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki”.
Ujio huu wa Kijenge umefanya Fanisi kuongeza wigo wake wa uwekezaji ambapo sasa ni miongoni mwa makumpuni nane yaliyopo mkoani Arusha ambayo yanajuhisisha na sekta mbalimbali ikiwemo za kilimo (hasa cha biashara), elimu, uuzaji wa bidhaa za rejareja kwa wateja(FMCG) pamoja afya.
Sehemu nyingine ambazo kampuni ya Fanisi imewekeza ni pamoja na Halton, duka la dawa za rejareja ambalo linapatika zaidi ya sehemu 30 jijini Nairobi, ambalo hivi karibuni limeingia ubia na Tuskys katika uhifadhi wa dawa katika maeneo yao; Hillcrest International Schools,  kundi la taasisi za kielimu zenye mrengo wa mtaala wa Kiingereza; Prodev Group, Kampuni ya usagaji na uuzaji mahindi iliyopo Rwanda; Sophar, duka la uuzaji na usambaziaji dawa la jumla lililopo nchini Rwanda;Live Ad, kampuni inayojiuhusha na matangazo ya nje iliyopo nchini Kenya na vilevile European Foods Africa Ltd, kampuni inayojiuhusisha na utunzaji na usambazaji wa vyakula ambayo kwa sasa inauza Piza, matunda na juisi asilia.
Kampuni ya Fanisi Capital ni kampuni ya uwekezaji miradi yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 50, ambayo inalenga kuzizibadilisha sekta mbalimbaliza kibiashara kama vile, Afya, Kilimo cha Biashara, Elimu na , Uuzaji wa bidhaa za rejareja kwa wateja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni