Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mama Elizabeth Chatham,
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Caniberra nchini Australia inayotoa
huduma ya Afya ya Mama, vijana na watoto mara baada ya kufika eneo la
hospitali kwa madhumuni ya kujionea namna bora yautoaji huduma. Mama
Salma yupo nchini Australia akifuatana na mumewe Rais Jakaya Kikwete
kwenye ziara rasmi ya kiserikali nchni humo.
Mke wa
Rais na Mama Salma Kikwete na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya CaniberraMama Elizabeth Chatham wakibadilishana mawazo
wakati walipokuwa wakitembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma ya
mama, vijana na watoto.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiwaangalia baadhi ya watoto wanapatiwa huduma
ya matibabu katika hospitali ya Caniberra wakijishughulisha na michezo
mbalimbali wakiwa na wazazi wao.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akimpa pole na kumtakia apone haraka binti
Addison Stephen,6, aliyevunjika mguu na kufungwa PoP na hatimaye kulazwa
hospitalini hapo huku akihudumiwa na baba yake Mzazi Bwana Stephen
Miles (aliyesimama kulia) na aliyechuchumaa ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali hiyo Mama Elizabeth Chatham.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akimbeba mtoto mchanga Isabella mwenye umri wa
siku moja aliyezaliwa na uzito wa kilo 3 na gramu 8 katika hospitali ya
Caniberra nchini Australia huku wazazi wake Bwana Steven Fanner,34, na
Bibi Tania Mras,32, wakishuhudia tarehe 28.7.2015.
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake,WAMA, Mama Salma Kikwete
akimkabidhi jarida linalochapishwa na Taasisi yake kwa Mama Elizabeth
Chatham, Mkurugenzi Matendaji wa Hospitali ya wanawake, vijana na watoto
ya Caniberra nchini Australia mara baada ya kutembelea sehemu
mbalimbaali za kutolea huduma hospitalini hapo yarehe 28.7.2015.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Mke wa Gavana Jenerali
wa Australia Mama Cosgrove mara baada ya Rais Kikwete kukutana na
Gavana Generali wa nchi hiyo Mheshimiwa Peter Cosgrove kwenye Ikulu ya
nchi hiyo tarehe 28.7.2015.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akitia saini kitabu cha wageni kwenye Ikulu ya
Australia huku Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mwenyeji wake Gavana
Jenerali Peter Cosgrove na Mkewe wakishuhudia.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni