Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose (katikati),
akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda wakati
akiwasili kwenye hafla ya kuzindua kisima cha maji safi katika Kituo cha
Watoto Yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka Dar es
Salaam jana.
DC Makonda akisaini katika kitabu cha wageni katika kituo hicho.
Mmoja wa vijana wa kituo hicho akiigiza igizo kuonesha changamoto zinazowakabili watoto waishio katika mazingira hatarishi.
Mkuu
wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Evans Tegete (kulia), akizungumza
katika hafla ya kuzindua kisima hicho. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose na Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Paul Makonda.
Naibu
Mkurugenzi wa Kituo hicho, Theobard Bubelwa (kulia), akiteta jambo na
Chief Commerial Officer wa Zantel, Sukwinder Bajwa wakati wa hafla hiyo.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose (kushoto),
akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,
Paul Makonda.
Watoto wa kituo hicho na wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Watoto wa kituo hicho wakitoa burudani.
DC Makonda akipokea risasi ya watoto wa kituo hicho.
Vijana wa kituo hicho wakitoa burudani.
DC Makonda akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alitoa ahadi ya kuwasomesha baadhi ya wanafunzi wa kituo hicho.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, akifungua pazia wakati akizindua
kisima cha maji katika Kituo cha Yatima cha Watoto Wetu Tanzania
kilichopo Mbezi Suka Dar es Salaam jana. Kisima hicho kimejengwa kwa
ufadhili wa Kampuni ya Simu ya Zantel.
DC Makonda akifungua bomba kuashiria uzinduzi wa kisima hicho.
Hapa DC Makonda akimtwisha maji mmoja wa wanafunzi wa kituo hicho baada ya kukizindua.
DC Makonda akimkabidhi kitabu, mtoto Yusla Omari kwenye uzinduzi huo.
DC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na timu nzima ya kituo hicho.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya Simu ya Zantel jana ilitoa msaada wa kisima cha maji kwa watoto
yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania,ikiwa na lengo la kumaliza
tatizo la maji na kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa
takribani watoto 70 wa kituo hicho.
Tatizo
la maji ni moja ya matatizo sugu katika mkoa wa Dar es salaam pamoja na
Tanzania kwa ujumla hivyo msaada huu ni wa muhimu kwa watoto wa kituo
hicho.
Kisima
hicho kilichokabidhiwa jana kitatoa maji safi na salama na yaliyotayari
kwa matumizi ambayo yatawasaidia watoto kuepukana na maradhi
yanayosababishwa na maambukizi ya maji yasiyo salama na machafu.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo , Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zantel,
Pratap Ghose alisema kampuni ya Zantel imekuwa siyo tu ikitoa huduma
bora na zenye unafuu kwa wateja wake bali pia imekuwa ikifanya jitihada
za kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwenye jamii inayoizunguka
‘Kampuni
yetu inalenga kugusa maisha ya wananchi wanaotuzunguka, na ndio maana
tumeamua kutoa msaada huu wa kisima ili kiweze kukisaidia kituo hiki
kumaliza moja ya matatizo yaliyokuwa yanawakabili kwa muda mrefu’
alisema Pratap.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika
shughuli ya makabidhiano hayo, aliipongeza kampuni ya Zantel kwa msaada
huo akisema ni ishara inayofaa kupongezwa.
‘Ustawi
wa watoto na vijana ni jambo muhimu katika jamii, hivyo nakipongeza
kituo hiki kwa kazi kubwa wanayofanya, na pia kampuni ya Zantel kwa
kulikumbuka kundi hili muhimu katika jamii, na ninatoa wito kwa
makampuni mengine kushiriki na kusaidia kituo hiki’ alisema Makonda.
Kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka jijini Dar es Salaam kilianzishwa mwaka 2001, kwa lengo la kuhakikisha watoto wasio na wazazi au walezi wanapata matunzo na elimu bora.
Akitoa
neno la shukurani Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania,Evance Tegete
alisema awali kituo kilikuwa na tatizo kubwa la maji, lakini sasa
shukrani kwa Zantel tatizo hilo limemalizika.
‘Awali
tulikuwa tunategemea maji kutoka DAWASCO ambayo upatikanaji wake si wa
uhakika,tunawashukuru Zantel wameweza kutusaidia kutatua tatizo hili’
alisema Tegete. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni