Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Arusha na Mbunge wa Africa Mashariki Mh.Bernard Murunya amabye alikuwa mgeni rasmi katika tukio la kukabidhi pikipiki,akimkabidhi moja ya Pikipiki kwa katibu jumuiya ya wazazi Wilaya ya Arusha Rehema Mohamed jana katika makao makuu ya chama hicho jijini Arusha, jumla ya pikipiki saba zilikabidhiwa kwa Wilaya saba katika Mkoa wa Arusha huku Mwenyekiti wa Taifa Abdalah Bulembo pamoja Baraza kuu Taifa wakifanya jitihada za kupatikana kwa Pikipiki hizo,katikati ni Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau akisoma risala fupi kwa mgeni rasmi ambapo katika risala yake alisema kuwa ugawanyi wa pikipiki hizo saba ni juhudi za Mwenyekiti Taifa Abdalah Bulembo pamoja na Baraza Kuu la Wazazi Taifa ,Tukio hilo ni la Jumuiya ya wazazi Nchi nzima la kuwakabidhi Makatibu wa Wilaya zote 161 pikipiki kwaajili ya kurahisisha utendaji wa kazi na kuboresha suala zima la usafiri ikiwa ni kuimarisha Chama cha Jumuiya zote
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Arusha na Mbunge wa Africa Mashariki Mh.Bernard Murunya akijaribu moja ya pikipiki alizokabidhi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni