Rais Donald Trump amemfukuza kazi
Kaimu Mwanasheria Mkuu Bi. Sally Yates aliyeteuliwa kushika wadhifa
huo wakati wa Barack Obama.
Ikulu wa Marekani imemtuhumu Bi.
Yates kwa kuisaliti Idara ya Sheria kwa kukataa kuunga mkono agizo la
rais la kuwapiga marufuku raia wa Mataifa ya Kiislam kuingia
Marekani.
Bi. Yates aliwaagiza wanasheria wa
Idara ya Sheria kutotetea agizo la kuzuia wahamiaji, kutokana na
kuona agizo hilo linakiuka sheria.
Rais Donald Trump akitia saini moja ya maagizo yake kwa kutumia mamlaka yake ya urais
Dana Boente ameteuliwa kushika kwa muda wadhifa huo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni