Mwana kijiji Amina Longitoti akiwa anatoa kero yake katika mkutano huo
Habari picha na Mahmoud Ahmad,Monduli Baadhi
ya wananchi wa wilaya ya Monduli wameitupia lawama halmashauri ya
wilaya hiyo na kusema kuwa inachochea migogoro ya ardhi na kuwanyima
baadhi ya wananchi amani ya kukaa katika vijiji vyao
Hayo
wamesema jana wakati walipokuwa wakifanya mkutano wa adhara uliofanyika
katika kijiji cha Lendikinya kilichopo ndaniya halmashauri ya
Monduli mkutano ambao uliohudhuriwa na vijana wa jamii ya Kimasai
(morani) na wazee wa mila (Laigwanani) zaidi ya 300, kueleza ardhi ya
kijiji hicho inayotaka kunyang’anywa na halmashauri hiyo,ambapo walisema
kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na uongozi huu mpya wa halmashauri ambao
unaongozwa na chadema kwani katika kipindi kilichopita walikuwa
hawanyanyaswi wala awafukuzwi katika maeneo yao ambayo walikuwa wanaishi
tangu enzi za mababu zao .
Mmoja wawananchi hao
aliyejitambulisha kwa jina la Songoyo Ole Matata alisema kuwa uongozi
wa halmashauri hiyo umekuwa ukiwasumbua na kuwafukuza katika maeneo hayo
ambayo ,walikaa tangu enzi za mababu wao,huku akibainisha kuwa pamoja
na kuwa wanafukuzwa lakini sio wananchi wote bali uongozi huo unafukuza
wananchi kulingana na chama ambacho anatokea.
“Tumekuja apa siku
nyingi lakini tunashangazwa hatujawai kufukuzwa ila tangu halmashauri
hii ichukuliwe na chadema tumekuwa tunanyanyaswa sana haswa sisi
tunaotoka na tunajilikana ni wanachama wa chama cha mapinduzi,nasema
hivyo kwa sababu hata sisi tunaolalamika ambao tumeambiwa tumevamia
msitu ni wanachama waCCM hamna mwanachama hata mmoja wa CHADEMA ambaye
amefatwa akaambiwa amevamia msitu ,mimi mwenyewe pembeni yangu
nimepakana na aliyekuwa waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa katika maeneo
hay o hayo kunashamba la Askofu Laizer lakini hao hawajaambiwa wamevamia
misitu waondoke ila sisi ambao ni wanachama wa CCM ndio tunaambiwa
tumevamia msitu kwakweli hii sio haki kabisa tunamuomba Rais wetu
magufuli aje atusaidie maana tunanyanyaswa sana”alisema Amina Longitoti
Akiogea
katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya
ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare alisema kuwa halmashauri ya
wilaya hiyo inayoongozwa na Chadema, inachochea migogoro ya ardhi na
chama chao hakitakaa kimya kwa hilo.
Alisema vijana wa
kimorani, Laigwanani na watu wengine akiwemo yeye mwenyewe Sanare,
wanamiliki ardhi iliyopo katika kijiji hicho kwa kufuata michakato yote
ya kisheria na hatimaye kupata hati ya kumiliki ardhi hivyo anashangazwa
na kusikitishwa na kauli ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Monduli, Isack Joseph kutangaza baadhi ya watu kuwa wanamiliki ardhi
katika msitu huo kinyume cha sheria.
Alisema CCM haitavumilia
uchochezi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa halmashauri kwa maslahi
binafsi na hatakuwa tayari kuona wananchi wananyanyaswa kwa sababu ya
maslayi ya mtu binafsi .
“mimi nilipata shamba hilo kama
mwananchi wa kijiji hicho na sikuchukuwa shamba hilo kama kiongozi wa
CCM hivyo nashangaa sana kwa kitendo cha kuingiza chama katika mambo
yangu binafsi kimenisikitisha sana na kwakweli sita vumilia kabisa na
kingine kinachonishangaza sio mimi tu au sisi tu ndio tunamashamba au
tunamiliki ardhi katika kijiji hichi kwani hata Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Chadema, Edward Lowassa (Waziri Mkuu mstaafu) ana ekari za kutosha
katika eneo hili pamoja na diwani wa Monduli Juu na wengine walioko
ndani ya Chadema lakini nashangaa wote amna aliyeambawa amevamia ila ni
sisi tu “alisema Sanare
Kwa upande mwananchi mungine
aliyejitambulisha kwa jina la Olais Taiyai alisema kuwa ubaguzi na
uchochezi uliopo ndani ya halmashauri hiyo unapaswa kupigwa vita na
hautavumilika hata kidogo kwani sio jambo jema linalofanywa na viongozi
hao na kuomba serikali kuingilia kati swala hili kwani wananchi hao
wanateseka na hawana pa kwenda iwapo wataendelea kufukuzwa katika
viwanja vyao
Naye Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya
Monduli, Amani Ole Silanga, aliwataka wanakijiji kuwa na subira, kwani
huo ni upepo mchafu unaovuma kupitia |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni