JANET JACKSON AONEKANA HADHARANI KWA MARA YA KWANZA TANGU AJIFUNGUE


Mwanamuziki Janet Jackson ameonekana kwa mara ya kwanza hadharani Jijini London akifanya manunuzi tangu ajifungue mtoto Eissa.

Janet Jackson na mumewe Wissam Al Mana walifanikiwa kumpata mtoto wao wa kwanza wa kiume Eissa wiki tatu zilizopita.

Janet alikuwa ameambatana na rafiki yake ambaye alikuwa amebeba mifuko yenye nguo za mtoto alizonunua kwenye duka hilo.

         Janet Jackson akiwa na rafiki yake aliyebeba mifuko yenye nguo za mtoto alizonunua

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni