Pichan ni Martin Mgallah ambaye ni Meneja mradi wa
Taasisi ya kuendeleza mifumo ya kimasoko katika kilimo Tanzania
(AMDT)Picha na Mahmoud Ahmad Manyara leo Blog 27 januari2017. |
Na.Mahmoud Ahmad,Arusha.
Taasisi ya
kuendeleza mifumo ya kimasoko katika kilimo Tanzania (AMDT)imewataka wakulima
kubadilisha kilimo kuwa biashara ,waondokane na kilimo cha kawaida na kuwa na
kilimo cha kisasa na kufahamu kilimo mkataba.
Hayo
yamesemwa na meneja mradi Martin Mgallah alipokuwa katika maonyesho ya zana za
kilimo Jijini Arusha na kusema kuwa wametenga zaidi ya dola za kimarekani
milioni kumi na tano kwaajili ya kuwawezesha wakulima katika zao la Alizeti
pekee ndani ya miaka
mitano (2016-2021)
“Taasisi
itamuwezesha mkulima kuongeza kipato chake cha mwaka kwa kubadilisha kilimo
kuwa biashara,tunaangalia pia mfumo wa masoko,tunamuwezesha mkulima kufahamu
kilimo mkataba yaani akishalima na kuvuna mazao yake asihangaike tena kutafuta
soko bali atauza mazao yake kwa bei nzuri,tunamuunganisha na soko moja
kwa moja”alisema
meneja mradi Martin.
Amesema
kuwa wakulima zaidi ya 60,000 watanufaika na mradi huo,huku akianisha mikoa
ambayo wataanza nayo ambayo ni pamoja na
Manyara,Shinyanga,Singida,Dodoma,Iringa,Njombe,Mbeya Songwe ,Katavi,Lindi,Rukwa
na Mtwara.
Martin
amesema kuwa lengo kubwa la( AMDT) kuhakikisha kuwa mkulima anazalisha kilicho
bora ,amesema mazao ambayo wataanza nayo ni Alizeti,mahindi,na jamii ya
mikundekunde katika mikoa tajwa.
Aidha
amesema kwaba wanampatia mkulima elimu sahihi,namna ya kulima kilimo
cha kisasa,kumuelimisha
mkulima kuwa na bima
itakayomuwezesha
kupata nyezo za kisasa za kilimo hivyo amewataka wakulima kuwatembelea ili
waone ni kwa namna gani wanaweza kunufaika na program hii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni