Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
akiwahutubia wananchi wa maeneo ya Ihungo Sekondari Mkoani Kagera  
hawapo pichani mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika 
Shule ya Sekondari Ihungo
 Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini 
Kitabu cha wageni pamoja na balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke 
mara baada ya kuwasili katika uwanja wa mkutano katika Shule ya 
Sekondari Ihungo
 Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
 jambo na Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu.
 Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa 
pamoja na balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke (kushoto) wakiweka
 jiwe la msingi katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo 
mkoani Kagera. Shule hiyo inajengwa upya kufatia kuathirika na tetemeko 
la Ardhi lililotokea mkoani humo.
 Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama 
wakati Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke alipokuwa akibonyeza 
kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya 
Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Wakwanza kushoto ni Waziri wa Elimu 
Profesa Joyce Ndalichako.
 Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na 
Balozi wa uingereza hapa nchi Sarah Cooke wakikagua ujenzi wa majengo ya
 Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera.
 Mtendaji
 Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Elius Mwakalinga akitoa maelezo 
ya mradi huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
 Magufuli wakati wa ukaguzi.
 Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
akisalimiana na Mbunge wa Bukoba mjini(CHADEMA) Wilfred Lwakatare mara 
baada ya kuwasili katika shule ya Sekondari Ihungo mkoani Kagera.
 Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
 na Charles Masinde mmoja wa wanachi mkoani Kagera aliyeamua kujenga 
nyumba yake mwenyewe mara baada ya tetemeko. Rais Dkt. Magufuli 
amemuahidi mwananchi huyo kuwa atampatia mabati 30 kwa ajili ya kuezekea
 nyumba yake.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni