Meneja biashara na mauzo wa DSE Patrik Msusa akiongea na waandishi wa habari mapema leo. |
Soko la hisa la Dar es
Salaam –DSE limesema kuwa ongezeko la hati fungani katika soko hilo limetokana
na baadhi ya wawekezaji kutafuta hathari ndogo zaidi za bei ya hisa.
Akizungumza na
wanahabari jijinia na Dar Es Salaam meneja biashara na mauzo Patrick Msusa
amesema kuwa hatua hiyo ya ongezeko la hati fungani limesababisha mauzo ya hisa
katika soko hilo kushuka kutoka shs 13.2 bilion mpaka kufikia shs 8bilioni.
“hatua hii pia imeweza
kusababisha makampuni matatu katika sekta ya mawasiliano kuingia katika orodha
ya makampuni ya simu yaliorodhoshwa katika soko letu la hisa, ikiwemo Vodacom,
Tigo na Airtel”. Alisema Patrick Msusa.
Vile vile ameongeza kwa
kusema kuwa, katika takwimu za soko hilo kwa kipindi caha wiki sita zilizopita
ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umeweza kupungua kwa asilimia 2.4% wakati kampuni ya TBL
ikiongoza kwa punguzo la asilimia 5% na sekta za kibiashara ikishuka kwa
asilimia 15.6% ambapo hatua hiyo imetokana na kushuka kwa hisa za benk ya CRDB.
Hata hivyo aliyataka makampuni
ya mawasiliano ya simu nchini kuweza kujiorodhesha kufuatia sheria ya serikali
ya kuyataka makampuni hayo kuuza hisa za zao kwa wananchi kupitia soko hilo ili
kukuza na kuchangia katika pato la taifa.
“Hadi sasa tunayo orodha
ya makampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi matatu tu hivyo basi napenda kutoa
wito kwa makampuni mengine kuweza kujiorodhesha katika soko letu”aliongeza
Msusa.
Msusa aliongeza kuwa
suala la kushuka kwa mauzo ya hisa
katika soko hilo limetokana na mdororo wa kiuchumi kwa siku za hivi karibu
kuliyo yakumba baadhi ya makampuni hapa nchini.
Mwisho………………….
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni