WAANDISHI WA HABARI ANDIKENI HABARI BILA WOOGA, RC GAMBO


Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akiingia ukumbini tayari kwa kuanza rasmi kwa kongamano na waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa maendeleo katika mkoa wa Arusha.picha zote na mahmoud ahmad arusha

Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa maendeleo katika komgamano hilo.
 Mkurugenzi wa Kituo cha mikutano cha kimataifa AICC Elishilia Kaaya akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria katika kongamano hilo na yeye kama mwenyeji wa eneo hilo akiwakaribisha katika kituo hicho.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano ambalo aliwaahidi waandishi kuwa ataliiitisha kwaajili ya kujadili na kupata taarifa ya maendeleo katika mkoa wa Arusha pamoja na wadaumbalimbali.
Mwenyekiti wa Arusha press club (APC) Akizungumza na katika kongamano hilo.
Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega akizungumza katika kongamano hilo .
Wa kwanza kushoto ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo ,akiwa kwenye kongamano katika kituo uliofanyika katika kituo cha kimataifa cha mikutano AICC katika ukumbi wa Mbayuwayu.
Wadau wa Utalii  kutoka TANAPA wakiwa katika kongamano la wadau wa habari mkoa wa Arusha .
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika kongamano hilo lililoitishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha ili kuangalia na kujadili maendeleo ya mkoa kwa ujumla.
Wa kwanza kushoto ni mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi Mussa Juma ,akifuatiwa na Omary Moyo wakiwa katika kongamano hilo.
Mgeni rasmi mkuu wa mkoa pamoja na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari waliohudhuria kongamano hilo.
Mwandishi wa habari wa kituo cha luninga cha chanel ten Jamillah Omary akiwa na mkurugenzi mwenza wa Me Production ambaye pia ni mpiga picha wa kituo cha luninga cha ITV Anold Rweyemamu.
Kutoka kulia ni  Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athuman Kihamia,aliyeko kushoto kwake ni mwenyekiti wa ccm mkoa ndugu Laizer




Na.
Mahmoud Ahmad, Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo Amewataka waandishi wa habari
kuandika habari zao bila wooga na wasiandike habari zinazowafuarahisha
viongozi pekee, badala yake kuandika kwa uhuru, lakini pia kuandika
habari za kweli  wala wasitake kuwafurahisha viongozi ilimradi habari
hizo ziwe za ukweli

 Aidha akazitaka taasisi za Serikali  na umma mkoani hapa  kutoa
taarifa kwa wakati ilikuondoa kero na kuweka majibu sawa kwa jamii
yatakayosaidia kuondoa manung’uniko yanaweza kumalizwa kwa kutoa
taarifa sahihi na kwa wakati kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakti
akifungua kikao cha wadau wa habari na taasisi za serikali lengo
likiwa ni kupata taarifa za mkoa wa Arusha kuhusu utendaji kazi kwa
kipindi cha nusu mwaka .

Ameongeza kuwa migogoro ya Ardhi mingi inachangiwa na wanasiasa
wanaotaka kuomba kura na mingine inachangiwa na wenyeviti wa vijiji
hali inayoonyesha kuwapo kwa migogoro isiyo isha maeneo yote mkoani
petu.

“ Naombeni Andikeni kwa uhuru habari zenu lakini za kweli wala hakuna
atakayewabugudhi,tukosoweni wala msitake kuwafurahisha viongozi,
lakini andikeni Ukweli kumekuwepo uandikaji habari nzuri za viongozi
tu andikeni habari za kukosoa ilikuweza kujisahihisha”.aliongeza Gambo

Ameongeza kuwa wananchi kupeleka malalamiko ya migogoro kwa viongozi
wa mkoa ni wazi  kuwa watendaji wa ngazi za chini kuanzia ngazi ya
wilaya na ngazi zingine hawafanyikazi ipasavyo,ambapo serikali itaanza
kuwashughulikia vinara wa migogoro ya Ardhi mkoani petu.
Ameongeza kuwa waandishi wa habari waandike habari zenye ukweli
zitakazo saidia kuondoa kero nao kuweza kujisahihisha zenye mwelekeo
wa kuwatumikia wananchi kwa kuacha Alama ya uongozi.

Ameutaka mfuko wa hifadhi ya Bima ya Afya kuhakikisha wateja wao
wanapata huduma bora na kujua matatizo wanayopata wateja wao kwenye
hospitali ya selian na kukaa na uongozi wa Selian kujua ni namna gani
mtayapatia ufumbuzi malalamiko yao, pia tembeleeni kwenye vyuo vikuu
vyote mkoani petu ili kujua malalamiko ya wanavyuo kuhusu huduma zenu.

“Watendaji wa serikali  timizeni  wajibu wenu katika kuwahudumia
wananchi na waelezeni ukweli hatua zinazochukuliwa kuondoa kero mbali
mbali na serikali yao kwani itasaidia kukuza ushirikiano na kuweza
kukuza maendeleo kwa wananchi”aliongeza Gambo

Nae  mkuu wa  wilaya ya Arusha  Gabriel Daqarro amewataka wanahabari
kuandika habari zao kwa weledi bila kumung’unya kwani zitaisaidia
serikali kuweza kutambua kero za wananchi na kuzipatia majawabu
yatakayosaidia kukuza na kuweza kujiletea maendeleo.

Ameongeza kuwa ushirikiano kati ya idara za serikali na wanahabari
zitasaidia kuweza kutoa taarifa ya utendaji wa serikali na
kijitathmini wapi tulipo na wapi tunakosea katika



Kwa upande wamafanikio utekelezaji wa mkoa kuanzia mwaka 2005 mkoa ulikuwa na shilingi 723,809 milioni kwa mwaka huo mkoa ulikuwa wa (9) katika kuchangia patao la Taifa,ambapo pato la mkazi lilikadiriwa kuwa shilingi 506,902 kwa mwaka sawa na shilingi 1,389 kwa siku.

 Kwa mwaka 2010 pato la mkoa wa Arusha lilikuwa shilingi 2,136,514milioni kwa kuchangia pato la taifa Arusha ilikuwa ya 7.mwaka huo pato la mkazi wa Arusha lilikuwa shilingi 1,283,361 kwa mwaka sawa na shilingi 3,516 kwa siku.

Hadi mwaka 2015 pato la mkoa linakadiriwa kuwa shilingi 4,271,447milioni.
 kwa takwimu hizo pato la mkazi wa Arusha lilikuwashilingi 2,322,031 milioni kwa mwaka ni sawa na shilingi 6,361 kwa siku.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni