Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden
amesema rais mteule Donald Trump anapaswa kukua, na amemkosoa
kuhusiana na hatua yake ya kushambulia vyombo vya Kiitelijensia.
Kauli hiyo ya Bw. Biden, ameitoa
huku Bw. Trump akitarajiwa leo kupata maelezo kutoka kwa vyombo vya
kijasusi vya Marekani kuhusiana na madai ya Urusi kuingilia uchaguzi
wa urais wa Marekani.
Bw. Biden amesema kwamba ni kutokuwa
na akili kwa rais mteule kutokuwa na imani na vyombo vya
Kiitelejinsia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni