Mkurugenzi wa kampuni ya Econnet Hashim Magessa akiongea na wanahabari hawapo pichani leo jijini Dar es salaam kuzungumzia kampuni hiyo kuanzisha Kanzidata ya Elimu kuisaidia serikali kutatua cha
Mahmoud Ahmad Dar es salaam
Tafiti
zilizotolewa na bank kuu ya dunia kupitia delivery indicators
imeonyesha kuwa 37% ya waalimu waliokutwa mashuleni hawakuwa madarasani
katika muda wa masomo hali inayopelekea kushuka kwa viwango vya elimu
nchini
Amesema hayo leo mkurugenzi mtendaji wa ECONNECT Bwn
Hashimu Magesa alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam
leo,ambapo amesema kuwa jambo hilo la kukosekana kwa waalimu madarasani
katika muda wa masomo linaashiria kuwa wanafunzi hawapati elimu kwa
kiwango kilichokusudiwa na wizara ya elimu na mamlaka yake
Ameongeza
kuwa pamoja na changamoto hizo za waalimu kumekuwepo na wanafunzi hewa
pamoja na utoro uliopitiliza hali inayopelekea kushuka kwa viwango vya
elimu kwa kutokujua kusoma na kuandika
Aidha Bwn Magese
amesema kuwa kutokana na changamoto hizo na nyinginezo zinazoikabioli
sekta ya elimu hapa nchini ndio maana taasisi ya ECONNECT imekuja na
mfumo huo wa Kanzidata utakao isadia serikali kutatua changamoto za
kielimu kwa ujumla
Amesema kuwa mfumo huo wa Kanzidata(DATABASE)utasaidia kuwa na takwim u sahihi zinazohusu kujua idadi shule,waalimu,wanafunzi,madarasa,madawati
nk pamoja na mkwamo wa mawasiliano kati ya utawala wa shule na
mzazi/mlezi utakaokuwa ukitoa taarifa kwa haraka juu ya maendeleo ya
haki elimu kwa mwanafunzi kupitia mawasiliano ya simu za kiganjano ambao
utagarimu shilingi mia tatu kwa ajili ya kupata huduma zote hizo
Bwn
Magesa amesema kutokana na utafiti wa majaribio walioufanya kwenye
wilaya ya ilala kwa jumla ya shule 152 ampo katika zoezi hilo
waliorodhesha taarifa mbalimbali za kielimu kupitia takwimu sahihi
ambazo kwa sasa zinawapa taarifa na kuokoa fedha ambazo zingetumika
kuchapisha taarifa na huku taarifa hizo zikifika kwa haraka kwa wahusika
Hta
hivyo taasisi ya ECONNECT imetoa wito kwa serikali kuutumia mfumo wa
majaribio kwa ndani ya mwaka mmoja ili kujiridhisha na ufanisi wake,pia
taasisi inawataka wadau mbali mbali wa elimu ikiwa ni pamoja na
makampuni,taasisi na watu binafsi kushirikiana kwa pamoja kwaajili ya
kuwezesha utekelezaji wa mfumo utakaosadia kuboresha elimu hapa nchini
kwa manufaa ya taifa letu kwa ujumla.ngamoto za kielimu picha na mahmoud ahmad dar es salaam | | | | | |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni