Ripoti ya Kiintelejensia ya Marekani
imesema rais wa Urusi Vladimir Putin aliamua kumsaidia Donald Trump
kushinda uchaguzi wa urais wa Marekani.
Ripoti hiyo imesema kuwa kiongozi
huyo wa Urusi aliagiza kufanyika kampeni yenye lengo la kujenga
ushawishi wa matokeo ya uchaguzi.
Baada ya kupewa taarifa hiyo rais
mteule Bw. Trump alisita kuishutumu Urusi kwa kitendo hicho na badala
yake alisema kuwa hata hivyo matokeo ya uchaguzi hayakuathiriwa.
Rais wa Urusi Vladmir Putin anashutumiwa kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni