PASS YAWATAKA WAKULIMA,WAFUGAJI NA WAVUVI KUFANYA SHUGHULI ZAO KITAALAM

Nicomed Bohai ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi  ya kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo Taifa  (PASS)picha zote na mahmoud ahmad


 Baadhi ya wakulima wakipata maelekezo katika Pass katika maonyesho ya zana za kilimo yaliyofanyika Jijini Arusha na kumalizaika jana maonesho hayo yalikuwa ya siku mbili.

Na.Mahmoud Ahmad, Arusha.
 
 Asasi ya kusaidia  sekta binafsi ya kilimo (Pass)imewataka wakulima na wajasiriamali wote wa kilimo ,uvuvi na wafugaji wafikirie namna ya shughuli zao kitaalam.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa asasi hiyo Nicomed Bohai ya kwamba wakulima wafikirie kufanya shughuli zao kibiashara,watafute elimu na maarifa ili waweze kudhaminiwa kupata mkopo wa kuendeleza shughuli zao.

Amesema kuwa  wanajenga mahusiano ya kibiashara  kutoka kwa wafanya biashara wakubwa kwenda kwa wadogo,ili wale ambao wameshapiga hatua wawainue wale ambao bado,kwa kutengeneza mchanganuo wa kibiashara na kutoa udhamini wa mkopo.

Aidha mkurufenzi huyo amesema kuwa Asasi hiyo ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo ipo tayari kumsaidia mtu binafsi,vikundi au makampuni kutumia huduma ya (Pass)haswa wajasiariamali binafsi amabao wana dira ambao wanafanya biashara katika hali ya ufanisi na kibiashara.

Sambamba na hayo amesema ya kwamba asasi hiyo inashirikiana na benki washirika zaidi ya 11 kupata mkopo kwa wakulima ambao wanaoweza kufikia angalau vigezo vya msingi kwaajili ya ukopaji,huku kipaumbele kikitolewa kwa wateja wenye matokeo makubwa katika mwendelezo wa mnyororo wa thamani kwa bidhaa za kilimo hususani katika mazao ya chakula ,biashara na mazao ya kusafirishwa nje ya nchi.

Ameainisha mikoa ambayo Pass ipo nchini Tanzania kuwa ni Mwanza ,Kigoma,Kilimanjaro,Morogoro,Mbeya, Dar-es- salaam na Mtwara,amesema wanatumia ofisi hizi za kanda ili kuwafikia wakulima kwa karibu zaidi.



.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni