Kushoto ni Katibu wa UVCCM wilaya ya
Longido Isaya Karakara, Katibu
Hamasa wa UVCCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel na Mjumbe Baraza Kuu
UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko w akikabidhi msaada kwa Mmiliki wa
kituo cha
kulelea Watoto yatima cha Masai Foundation Joyce Kabati
Kushoto ni Katibu wa UVCCM wilaya ya
Longido Isaya Karakara, Katibu
Hamasa wa UVCCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel na Mjumbe Baraza Kuu
UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko w akikabidhi msaada kwa Mmiliki wa
kituo cha
kulelea Watoto yatima cha Masai Foundation Joyce Kabati
habari picha na Mahmoud Ahmad,Arusha.
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Longido
umetembelea kituo cha Watoto yatima na Wanaoishi katika mazingira magumu cha
Masai Foundation kilichopo mji mdogo wa Namanga na kutoa msaada wa vyakula
pamoja na vifaa mbalimbali.
Mjumbe Baraza Kuu
UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko Amesema kuwa wameamua kushirikiana na
jamii katika kusaidia watoto ikiwa ni moja kati ya michango wanayoitoa ili
kutosheleza mahitaji muhimu yanayohitajika katika kituo hicho.
Robert Amesema kuwa jukumu la kuwasaidia watoto yatima na
wanaoishi katika mazingira magumu ni la kila mwanajamii hivyo jamii inapaswa
kujitoa kusaidia watoto hao.
Katibu Hamasa wa CCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel amesema
kuwa vijana hao wameamua kujitoa kutoa msaada kwa jamii ili kusaidia watoto
wanaoishi katika mazingira magumu hivyo ameiomba jamii kujitokeza kwa wingi
kuwasaidia watoto hao.
“Hawa ni watoto wetu sote kila mtu anapaswa kuona kuwa ana
jukumu la kuwasaidia hawa watoto ili waweze kufanikisha ndoto zao” Neema
Katibu wa UVCCM wilaya ya Londigo Isaya Karakara na
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya Tulli Lemanga aliyejitolea kuwakatia bima
ya afya watoto wanaolelewa katika kituo hicho wamesema kuwa vijana hao wataendelea na utamaduni huo
mara kwa mara katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua changamoto
za watoto.
Mmiliki wa kituo
hicho Joyce Kabati amewashukuru vijana hao kwa kutembelea watoto hao jambo
ambalo linaleta faraja kwa watoto hao ambao na wanamahitaji mbalimbali ambayo
yamewasilishwa na vijana hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni