Dar
es Salaam. Vigogo wawili wa siasa za upinzani nchini, Edward Lowassa na
Maalim Seif Sharif Hamad kesho watapanda jukwaani katika Skuli ya
Fuoni, Zanzibar kumnadi mgombea ubunge Jimbo la Dimani kwa tiketi ya
CUF, Abdulrazaq Khatib Ramadhan.
Katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Lowassa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa
zamani na Maalim Seif aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
katika Serikali iliyopita, waligombea urais wa Jamhuri ya Muungano na
Zanzibar, mtawalia.
Uchaguzi
huo wa Dimani, utafanyika Jumapili Januari 22, kujaza nafasi iliyoachwa
na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Hafidh Ally Tahir aliyefariki dunia
Novemba 11, mwaka jana katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Chini
ya ushirikiano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), jana Chadema kilitangaza utaratibu jinsi vigogo wake
watakavyoshiriki kampeni za uchaguzi huo kwa staili tofauti ili
kuhakikisha mshirika wake CUF anaibuka kidedea.
Naibu
Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu alisema jana kwamba kesho,
Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu, atakuwa kiongozi wa kwanza
wa Chadema kuhudhuria kampeni hizo akishirikiana na Maalim Seif ambaye
pia ni Katibu Mkuu wa CUF.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni